Tuesday, January 7, 2020

MAUAJI NDANI YA KIJIJI CHA KEDDIE

SEHEMU YA 13

MARTIN SMARTT alielezea suala la nyundo yake kupotea siku mbili kabla ya mauaji ila halikufuatiliwa hili na DOUG THOMAS, zile shahidi zilizokutwa kwenye mauaji baada ya FBI kuzichunguza hakukutwa na alama zozote ila Kuna kipande cha “medical tape” kilibakiza alama na DOUG THOMAS kufunika kombe kama kawaida kwa kubaki nacho ofisini kwake

kombe la mwisho alilofunika afande DOUG THOMAS ilikuwa ni ujumbe ambao aliandika MARTIN SMARTT kwenda kwa mkewe baada ya kutendeka mauaji alivyoondoka na BOUBEDE kwenda kijiji kingine cha RENO.

sehemu ya ujumbe huo ulikuwa ukisema “nimelipa gharama ya penzi lako na sasa nimelinunua kwa uhai wa watu wanne” ila ujumbe huu haukutumika kama ushahidi wa kuweza kumtuhumu MARTIN SMARTT na hii ni kazi ya DOUG THOMAS.

ujumbe huu umekuja kutumika kama ushahidi katika karne ya 21 wakati kijiji cha KEDDIE kikiwa chini ya afande MIKE GAMBERG kama mpelelezi mkuu na alikosoa upelelezi wa zamani wakati tukio hili limetokea wakati huo afande huyu alikuwa na maiak 16 na anaijua familia ya SHARP vizuri sababu na yeye ni mkazi wa huko.

sababu kesi hii inaendelea ujumbe huu umeunganishwa kwenye ripoti ya uchunguzi na imekuja kuleta shida kidogo sababu ya MARYLN SMARTT kuhojiwa na wapelelezi kuhusu mwandiko wa ujumbe huo kama ni wa mumewe na kusema hakumbuki mwandiko wa mumewe ni zamani sana aliona mwandiko wa mumewe na hana barua yoyote aliyosalia nayo iliyoandikwa na mumewe ili wafananaishe mwandiko.

hayo ni baadhi ya makosa yanayoonekana kufanywa na DOUG THOMAS kumlinda rafiki yake MARTIN SMARTT na kupelekea kesi kuwa ngumu na kuumiza vichwa wanausalama na afande DOUG THOMAS alihojiwa kujibu shutuma hizi kabla hajafa na kusema hakuwa rafiki wa MARTIN SMARTT na kweli alimhoji mwanzoni kabla ya FBI na alifauli kipimo cha LIE DETECTOR TEST na FBI nao walivyomfanyia akafaulu pia kuonesha sio muhusika wa mauaji.

kujikanyaga kote huko MARTIN na BOUBEDE ila afande DOUG THOMAS anasema walifaulu kipimo hicho inawezakana aliwapanga namna ya kujibu maswali pale FBI walipowahoji ndo maana wakafaulu yote yawezakana maana ni kweli kwenye ripoti ya FBI walifaulu.

kukaja kutokea mtaalamu wa saikolojia ambaye alidai kuwa MARTIN SMARTT alikuwa mgonjwa wake wa mambo ya saikolojia na alikuwa akimshauri aondokane na ugonjwa wa PTSD ni kweli MARTIN SMARTT alikuwa akionekana kufika kituoni kwa mtaalamu huyo.

sasa mtaalamu huyo anasema kuwa MARTIN SMARTT alikiri mbele yake kuwa alihusika na mauaji ya familia ya SHARP na kudai aliua SUE SHARP na TINA SHARP ila wale vijana hakuwaua yeye na hajui nani aliwaua na sababu kuu ya kutenda mauaji hayo ni kulinda ndoa yake ambayo ilikuwa ikiingiliwa na SUE SHARP kumshauri hasi mkewe.

wapelelezi nao maelezo haya wakayatumia kama sehemu ya uchunguzi ila hayana uzito kwasababu ni maneno hakuna ushahidi kama kweli MARTIN SMARTT alisema hata kama wamejiridhisha kuwa MARTIN SMARTT alikuwa mteja wake.

kufikia mwaka 2018 MIKE GAMBERG alisema na vyombo vya habari kuwa kwa msaada wa DNA kwenye kile kipande cha “medical tape” ambacho hakikutumika kama ushahidi zamani kwa kuonekana kufichwa au kudharauriwa na wanausalama wa KEDDIE kimeonesha kuwa muhusika wake mwenye hiyo DNA yuko hai na uchunguzi unaedelea ili kumtambua ni nani.

ikumbukwe washtumiwa wakuu yani MARTIN na BOUBEDE wameshakufa ila kwa mujibu wa DNA inaonesha mtuhumiwa bado yuko hai ndo maana upelelezi mgumu sana ukisema ukimbilie kuhitimisha kuwa MARTIN na BOUBEDE ndo wahusika unakuja kuaibika labda sio wao au ni mshirika wao mwingine kwa kusema walikuwa zaidi ya wawili au ndo wale watu tofauti kabisa na MARTIN na BOUBEDE ambao mtoto JUSTIN aliwaona na kuwaelezea FBI, yote ni kitendawili tuwaachie wapelelezi waendelee na kazi yao.

Kwa sasa kesi hii inabaki kama “UNSOLVED MURDER” mpaka pale wanausalama watakapokuja kuhitimisha ukweli wake tuendelea kusubiri kwani uchunguzi unaendelea.

kupitia kisa hiki kumeweza kutengenezwa filamu mbili za “THE STRANGERS” na “CABIN 28”.

Hiyo picha hapo juu ni barua (ujumbe) unaodaiwa kuandikwa na MARTIN SMARTT kwenda kwa mkewe...!!!!

MWISHO...!!!!

imeandaliwa na COMRADE SABOUR.
I
Continue reading

MAUAJI NDANI YA KIJI CHA KEDDIE

SEHEMU YA 12

Ufuatiliaji wa simu ile hukusaidia lolote sababu walishidwa kumpata nani aliyepiga ile namba na kuendelea na chunguzi zao bila mwanga wowote na washtumiwa wakuu wa mauaji yani MARTIN SMART na BOUBEDE waliamua kuhama kijijini KEDDIE kwa kupewa ruhusa na afande DOUG THOMAS..

kwa MARTIN SMARTT kuhamia mjni KLAMATH na BOUBEDE kurudi zake CHICAGO na BOUBEDE akiwa amerudi nyumani alitenda uhalifu na kutiwa gerezani na kabla ya hukumu yake alifariki mwaka 1988 akiwa jela na kuonesha kweli alikuwa kwenye mtandao wa MAFIA.

MARTIN SMARTT naye akaja kufariki mwaka 2000 kwa kansa na washtumiwa wakuu ambao wengi bado wanahisi walikuwa na uhusika na mauaji ya familia ya SHARP walikufa wakati upelelezi ukiendelea kwa FBI kutokata tamaa wakijua labda wanaweza kutambua wahusika wa mauaji.

FBI mpaka leo hii wameshindwa kutambua wahusika wa mauaji ya familia ya SHARP ilihali kulipatikana shahidi zilizotumika katika mauaji hayo na kushindwa huku kwa FBI na mapolisi wa kijijini KEDDIE kumezungukwa na sintofahamu ambazo zinamlenga mkuu wa kituo kijiji KEDDIE bwana DOUG THOMAS.

Afande DOUG THOMAS pamoja na polisi wake kijijini KEDDIE walihusika kuifanya kesi hii iwe ngumu kwa kushindwa kutatulika mpaka leo hii, afande DOUG THOMAS na MARTIN SMARTT ni marafiki wakubwa sana mpaka saa zingine MARTIN SMARTT na mkewe wakigombana wanapelekana mpaka kwa afande huyu kusuluhishwa.

wakati tukio la mauaji limetokea hawa maafande ndo walikuwa wa kwanza kufika eneo la mauaji kabla ya FBI na kuonekana kuvuruga ushahidi mzima eneo la tukio na kwenye Nyanja za upelelezi ukivuruga ushahidi basi kila kitu kinakuwa kimeharibika.

kwahiyo FBI kuja walichukua ripoti za DOUG THOMAS kuwaongoza kwenye uchunguzi sababu walikutia tayari wanausalama wenzao wameshaanza uchunguzi na ilikuja kujulikana kabla ya FBI kuwahoji MARTIN SMARTT na BOUBEDE tayari walishahojiwa na DOUG THOMAS.

ripoti iliyokuja kubainika kuonesha mahojiano ya DOUG THOMAS na washtumiwa wa mauaji ilikuwa ni vituko kama, BOUBEDE kwenye mahojano alisema kuwa alikuwa polisi wa CHICAGO kwa miaka 18 kitu ambacho ni cha uongo ila DOUG THOMAS alishidwa kukibaini au alipuuzia au alijua ukweli wake yote yawezekana wakati utaratibu wa kiupelelezi ni lazima DOUG THOMAS angepiga simu CHICAGO kujiridhisha kama BOUBEDE alikuwa polisi huko ila hakufanya hivyo na inawezakana alifanya hivyo makusudi sema akafukia kwa faidi zake binafsi.

kingine BOUBEDE alidanganya kwa kuongeza wiki mbili za kuwa ndo muda alioishi kijijini KEDDIE nalo DOUG THOMAS hakulifuatilia na mapolisi wenzie, BOUBEDE akadanganya tena kuwa MARYLN SMARTT ni mpwa wake wakati hawajuani kabisa ila DOUG THOMAS akafunika.

BOUBEDE alisema kuwa wakati wanarudi kwa mara ya pili nyumbani MARLYN SMARTT alikuwa macho kitu ambacho ni uongo, BOUBEDE alisema kuwa hajawahi kukutana wala kumjua SUE SHARP ni kitu ambacho ni uongo ila DOUG THOMAS akafunika.

MARTIN SMARTT alisema kuwa mtoto wake wa kambo JUSTIN EASON kuna kitu aliona siku ya mauaji ila DOUG THOMAS hakutaka kuhoji kujua hili kwa undani sababu wakati anasema hili JUSTIN EASON bado alikuwa ameshikilia msimamo wake kuwa hakusikia lolote usiku wa mauaji.

INAENDELEA....!!!!

SEHEMU YA 11

Huo ulikuwa ushahidi wa JUSTIN EASON kwa FBI na baada ya mchoro kukamilika alioneshwa hizo picha zilivyotoka na kusema wanafanana na huo mchoro na FBI wakautumia huo mchoro wa picha kwenye chunguzi zao kama watabahatika kumpata mtu anayefanana na huo mchoro.

Ushuhuda alioongea JUSTINE EASON hauaminiki asilimi 100 kwasababu mara kwanza alikataa kuwa hakusikia lolote ila safari hiyo amekubali na kuelezea hivyo ila mwisho wa siku FBI mchoro wa hao wauaji haukuwasaidia kwani hawakupata mtu anayefanana na hao.

FBI wakaendelea kinyonge na pelelezi zao huku wakiwa hawana mwanga wa mauaji ya familia ya SHARP wala kumpata TINA SHARP, kuingia mwaka 1984 tarehe 22 aprili muokota makopo mmoja katika kaunti ya BUTTE aliokota kipande cha fuvu.

Muokota makopo huyu akaamua kukipeleka hicho kipande cha fuvu polisi na mkuu wa polisi kaunti ya BUTTE alitangaza kwa vyombo vya habari kuwa kumeokotwa kipande cha fuvu na uchunguzi wake unafanyika kujua ni fuvu la binadamu au mnyama ili hatu zingine ziendelee ila kimuonekana ni fuvu la binadamu sema lazima wachunguzi wa kitabibu wathibitishe hilo.

Wakati tangazo hili limesambaa kote mkuu huyu wa polisi akapigiwa simu na mtu asiyemjua na kumwambia kuwa kipande hicho fuvu ni cha mtoto mmoja aitwaye TINA SHARP wa kijijini KEDDIE na kuendelea kuongea kuwa eneo hilo lina mabaki mengine ya TINA SHARP na simu ikakatwa..

Mkuu wa polisi alishangazwa na simu hiyo na kumbukumbu ya kesi hiyo ikamjia kwasababu ilikuwa habari ya nchi kwa kila mmoja kuongelea na kufuatilia kesi hiyo na haraka akawasiliana na FBI ili kuwalelezea kuhusu ujumbe wa simu hiyo.

FBI haraka wakafika na kuelekea eneo kulikookotwa fuvu na ukaguzi ukaanza mara moja na kweli baada ya ukaguzi walifanikiwa kupata mabaki mengine ya binadamu pamoja na blanketi, jaketi na suruali ambavyo ni mali za TINA.

FBI wakafikisha mabaki hayo pamoja na lile fuvu kwa wachunguzi wa kitabibu na kuwataka kukimbiza uchunguzi kama vinahusiana na TINA na baada ya uchunguzi matokeo yakatoka na kuonesha mabaki hayo yote ni ya TINA SHARP.

Mabaki hayo yalifikikaje, nani aliyaleta, alikufaje inabaki kitendawili kwa wapelelezi na kutoka hapo mabaki yalipokutwa mpaka Kijiji KEDDIE ni umbali wa kilomita 160 kwahiyo ni safari mtoto TINA alipelekwa kuuwawa huko.

Wapelelezi walikuwa wakijiuliza maswali magumu ni kwanini TINA SHARP apelekwe kuuwawa mbali tofauti na wenzie au ubakaji ulifanyika kwanza kabla ya mauaji yote bado ni maswali magumu na FBI wakarudia kufuatilia ile simu iliyopigwa kwa mkuu wa polisi ili asaidie upelelezi Kama sio muhusika mmojawapo wa mauaji ya kijijini KEDDIE.

Hiyo picha hapo juu ni mchoro wa hao wanaume kwa maelezo kutoka kwa mtoto JUSTIN...!!!!!

INAENDELEA....!!!!!
Continue reading

MAUAJI NDANI YA KIJIJI CHA KEDDIE

SEHEMU YA KUMI

Kadri  muda unavyozidi kwenda ndo matumaini ya kumpata hai yanapungua na wakati utafutwaji wake unaendelea na chunguzi za kujua wauaji wa familia ya SHARP yule mtoto mdogo kutoka familia ya SMARTT aliyekuwa amelala na watoto wenzie akaja na mpya kuhusu usiku wa mauaji

Mtoto JUSTIN EASON alisema kuna kitu anakumbuka kuhusu usiku wa mauaji na alimwambia hivyo mama yake na kubidi kuwataarifu FBI ambao haraka walifika nyumbani kwake na kumchukua kwa ajili ya mahojiano naye.

Ikumbukwe mara ya kwanza JUSTIN EASON na watoto wengine wa familia ya SHARP walisema hawakusikia chochote usiku ila safari hii mtoto JUSTIN EASON peke yake amekuja na jambo ambalo FBI linaweza kuwasaidia katika chunguzi zao.

JUSTIN EASON akaanza kuhadithia FBI kuwa usiku wa mauaji alisikia kelele ambazo zikamuamsha na kuangalia wenzake wawili bado wamelala na kuamua kuamka kwa kwenda mlangoni na kuufungua polepole ili aweze kuchungulia sababu ya hizo kelele.

Kuchungulia akamuona SUE SHARP akiwa amelala kwenye sofa huku wanaume wawili wakiwa wamesimama katikati ya sebule, FBI wakamuuliza aliweza kuwatambua hao wanaume na JUSTIN EASON akawajibu kuwa hapana na FBI kumtaka awaelezee wanafananaje.

Katika hilo jopo la maafisa wa FBI kulikuwa na maafisa ambao ni wataalamu wa kuchora wakielezewa sifa za mtu na JUSTIN EASON akaanza kuelezea sifa za hao wanaume na FBI wakawa wanajaribu kunukuu huku wengine wakichora ili wamuoneshe huyo mtoto kama walikuwa wakifanana hivi.

JUSTINE EASON akaendelea na kusimulia usiku wa mauaji, gafla DANA na JOHN SHARP wakaingia ndani ya nyumba [inaonekana ndo muda ule wanatoka kwenye sherehe usiku na kuonekana na familia ya SEABOLT] na hapohapo wakaanza kulumbana na wanaume hao.

Kulumbana kidogo vijana hao wakataka kupimana nguvu na wanaume hao ila haikuwa rahisi kwasababu wenzao walikuwa na silaha na JOHN SHARP akadhibitiwa huku DANA kuona mwenzie yuko chini ya ulinzi akajaribu kukimbia kupitia jikoni ila mwanaume mmoja ambaye alikuwa na nywele za kahawia na mabuti ya jeshi akamuwahi kwa kumrushia nyundo ambayo ilimpiga na kuanguka chini na kurudishwa wenzie waliko.

Wote wakaanza kufungwa ili wasulubiwe na wakati zoezi hilo la ufungaji likikamilika mtoto TINA SHARP akawa ametoka chumbani kwake akiwa na blanketi huku akiuliza kuna shida gani na bado alionekana yuko usingizini.

Mwanaume mmojawapo akamuwahi kumkamata TINA SHARP na alipojaribu kupiga kelele akazibwa mdomo na kuondoka naye kuelekea mlango wa nyuma na mwanaume huyo kurudi bila TINA SHARP na mateso ya kusulubu yakaanza rasmi na uoga ukamwingia JUSTIN EASON na kukimbia kitandani kulala.

INAENDELEA...!!!!
Continue reading

MAUAJI NDANI YA KIJIJICHA KEDDIE

SEHEMU YA TISA

Baadae mchana MARTIN SMARTT na rafiki yake wakarudi nyumbani na kila mmoja hasira zilikuwa zimepungua na kuanza kuongea vizuri bila kujibishana na wakala pamoja huku MARTIN SMARTT akimuulizia mtoto na kuambiwa yuko kwakina familia ya SHARP.

Kufika jioni MARTIN SMARTT akamwomba mkewe waende kilabu cha hapo jirani kiitwacho BACK DOOR ambacho pia MARTIN SMARTT ni mfanyakazi katika kilabu hicho na mkewe akakubali na waliondoka pia na BOUBEDE.

Wakati watatu hawa wametoka wakapita nyumbani kwa SUE SHARP na kumwambia kwanini wasijumuike naye kwenda kunywa jioni hiyo ila SUE SHARP akakataa kwa kuwashukuru ofa yao na wakaondoka zao kuelekea kilabuni [bar].

Wakiwa kilabuni hapo wakaanza kunywa na pombe kukolea kidogo MARTIN SMARTT akaanza mambo yake ya ajabu kwa kulalamika mziki unaopigwa ni mbaya anataka zipigwe nyimbo anazotaka yeye na maneno haya anamuambia meneja wa kilabu.

Meneja wa kilabu sababu anamjua vizuri MARTIN SMARTT akampuuzia na kumzidisha kumkasirisha na siku hiyo MARTIN SMARTT alikuwa mapumzikoni kilabuni hapo, baada ya kuona amepuuziwa akawaamuru wenzie [BOUBEDE na mkewe] waondoke kurudi nyumbani.

Wote kufika nyumbani bado MARTIN SMARTT analalamika kuhusu kupigwa nyimbo mbaya pale kilabuni na mkewe naye sababu anajua hakutaka kushughulika naye akawasha luninga na kuanza kuangalia mpaka kufika muda wake wa kulala akaamua kwenda zake kulala na kuwaacha MARTIN na BOUBEDE.

Mke wake kwenda kulala MARTIN na BOUBEDE wakarudi kilabuni tena na kuanza kulalamika vile vile kuwa miziki inayopigwa ni mibaya na akapuuziwa tena na hawakukaa sana wakaondoka, huu muda walivyoondoka haijulikani walienda wapi wawili hawa na mkewe anasema mpaka anastuka usiku sana mumewe akawa hajarudi ila kustuka alfajiri akamkuta mumewe yuko kitandani na hajui muda halisi aliorudi.

Asubuhi yake wakati ndo kunagundulika mauaji MARTIN SMARTT na BOUBEDE walikuwa wametoka hiyo asubuhi sana na kuelekea kijiji kingine na kurudi jioni, huyu BOUBEDE kwa mujibu wa MARTIN SMARTT anasema kuwa walikutana hospitalini wakati anaenda kliniki ya matibabu PTSD.

Urafiki wao ulianzia hapo hospitalini na kuja kumualika aje akae kwake kwa wiki kadhaa na huyo BOUBADE ana historia mbaya kidogo kwa kujulikana ni zao la familia mojawapo ya KIMAFIA ipatikanayo CHICAGO.

Katika familia hiyo ya KIMAFIA bwana BOUBADE anajulikana kama “MAN MADE” hii ilitia wasiwasi uhusika wa MARTIN SMARTT na mauaji ya familia ya SHARP ila FBI walishindwa kuthibitisha madai hayo kuwa BOUBEDE ni MAFIA.

Pia kitendo cha MARTIN SMARTT na mwenzie kufaulu mtihani wa LIE DETECTOR TEST ilibidi kuwaondoa hao katika washtumiwa na kuendelea na chunguzi zao huku bado wakiwa jambo linalowaumiza kichwa sana kuwa TINA SHARP yuko wapi maana wanamtafuta kila kona bila mafanikio na matangazo kibao kila kona ili kama kutatokea msamaria mwema kuweza kumtambua.

Hiyo picha hapo juu ni kilabu cha BACK DOOR...!!!

INAENDELEA....!!!!
Continue reading

MAUAJI NDANI YA KIJIJI CHA KEDDIE

SEHEMU YA NANE

MARYLN SMARTT anasema kuwa imefanana na hiyo nyundo kwasababu polisi walimuonesha hiyo nyundo iliyokutwa eneo la mauaji na kufanya FBI wageuze akili kwa huyo mama na ikumbukwe katika wale watoto waliopona ndani ya nyumba ya SUE SHARP mmojawapo ni mtoto wake aitwaye JUSTINE.

FBI wakaanza kumhoji MARYLN SMARTT na pia kwenda kukagua kwake nyumba nzima na katika mahojiano na FBI alisema kuwa anahisi mumewe MARTIN SMARTT anaweza kuwa muhusika katika mauaji ya familia ya SHARP.

MARYLN SMARTT aliendelea kusema kuwa hapo nyumbani pia amekuja mgeni siku chache kabla ya mauaji kutokea na hamuelewi vizuri na FBI kuona ni vyema nao wahojiwe haraka wanaweza kweli kuwa wahusika.

FBI wakamhoji MARTIN SMARTT na rafiki yake aitwaye BO BOUBEDE kuhusika na mauaji ya familia ya SHARP na baada ya mahojiano marefu kwa kutumia pia kifaa cha POLYGRAPH TEST marafiki hawa waliweza kufaulu kwa kuonekana hawahusiki ila ikumbukwe POLYGRAPH TEST haitoi majibu ya asilimia 100.

Kwanini MARTIN SMARTT na rafiki yake wahisiwe kuhusika na mauaji ya familia ya SHARP na mtu aliyekwenda kumshtumu ni mke wake ingawa kweli nyundo ilipotea ndani kwao ambayo inafanana na ile nyundo iliyotumika kwenye mauaji.

Turudi nyuma kidogo kwenye mahusiano ya familia hizi mbili za SHARP na SMARTT pamoja na usiku wa mauaji, familia hizi mbili zilihamia kwa kipindi kimoja kijijini KEDDIE huku upande wa familia ya SMARTT kuwepo na ugomvi wa mara kwa mara.

MARYLN SMARTT alikuwa akilalamika mumewe kumpiga na kumuonea wakati wa ugomvi wao na mtu pekee MARYLN alikuwa rafiki yake sana wa kumwambia mambo yake ni SUE SHARP na ushauri mkubwa aliokuwa akimpa rafiki yake kuhusu ndoa yake ulikuwa hasi.

SUE SHARP alikuwa akijaribu kujitolea mfano kwa rafiki yake kuwa amezaa watoto wengi na mumewe ila walipokuwa wanashindwana mara nyingi akafikia uamuzi wa kuachana naye kwa kufikishana kwenye vyombo vya sharia na talaka kutolewa kila mtu kufanya mambo yake na kubaki kama wazazi tu.

Sasa MARLYN SMARTT akiwa kwenye ugomvi na mumewe akipewa ushauri huo anaonekana kusikiliza na kuahidi kuutendea kazi ila ugomvi ukishaisha na mambo kwenda vizuri na mumewe basi anasahau kila kitu na mbaya zaidi anamuelezea mumewe kuhusu anavyoshauriwa na SUE SHARP.

Mwisho wa siku MARTIN SMARTT akawa anamchukia SUE SHARP kutokana na kumshauri hasi mkewe kuhusu ndoa yao na hiyo chuki ilikuwa wazi kwa mkewe MARLYN SMARTT, twende sasa kuona siku ya mauaji yani tarehe 11 aprili 1981 ilivyokuwa upande wa familia ya SMARTT.

Asubuhi ya tarehe 11 aprili 1981 nyumbani kwa SMARTT kuliamka kukiwa hakuko shwari kwa wanandoa hawa kuanza kugombana bila kujalisha uwepo wa mgeni BO BOUBEDE na kama kawaida yake MARLYN SMARTT akakimbilia nyumbani kwa SUE kujiliza na kuomba ushauri.

SUE SHARP kama kawaida yake akamshauri hasi kuhusu ndoa yao na baadae kurudi nyumbani na mumewe kuendelea na gubu kwanini alikimbilia huko kwa SUE SHARP na kujibiwa vibaya na mkewe kuwa SUE SHARP ndo mshauri wake na safari hii lazima atekeleze ushauri wake.

Hii kauli ilimkera sana MARTIN SMARTT na kuamua kuondoka zake na rafiki yake nyumbani hapo, mtoto JUSTINE alivyoombewa kushinda na kulala huko kwanina SHARP ilikuwa ahueni kwa MARYLN SMARTT sababu hakupenda mwanae aone ugomvi wao kwasababu akienda kwa baba yake mzazi anamuhadithia kinachompata mama yake.

Hiyo picha hapo juu unaweza kuona picha ya MARTIN SMARTT kwenye kitambulisho chake...!!!!

INAENDELEA....!!!!
Continue reading

MAUAJI NDANI YA KIJIJI CHA KEDDIE

SEHEMU YA SABA

Majirani wa SHARP wakaanza kuhojiwa kama walisikia lolote na kila mmoja alisema kuwa hawakusikia lolote zaidi ya bwana na bibi SEABOLT ndo walisikia sauti isiyoeleweka wakajua ni za wale vijana ndo wanarudi kutoka kwenye sherehe kumbe yawezakana ndo sauti ilikuwa ikitoka nyumbani kwa SUE SHARP baada ya kuvamiwa na wauaji.

Sasa mapolisi wakawa wanajiuliza kama sauti iliweza kusikika mpaka kwa jirani SEABOLT na kuwakera imekuwaje watoto wameshindwa kuisikia ila wakapotezea na kingine kilishowangaza kwanini wauaji waliamua kuacha silaha zao za mauaji eneo le tukio ili iweje na kumchukua TINA SHARP kwasababu gani..? yote yakawa maswali magumu kwa wakati huo.

Afande mkuu kijijini KEDDIE aitwaye DOUG THOMAS ambaye naye alikuja eneo la tukio alipiga simu juu kuomba msaada wa kiuchunguzi zaidi kuhusu tukio la mauaji kijijini kwake na maafisa wa FBI wakatumwa kwenda kijijini KEDDIE kupambana na kesi hii.

FBI kufika kijijini KEDDIE walichukua ripoti za uchunguzi w awali kutoka kwa afande mkuu DOUG THOMAS ambazo zilikuwa zimeambatanishwa na ripoti za kitabibu baada ya miili ya kina SUE, JOHN na DONA kufikishwa hospitalini.

Ripoti ya kitabibu ilisema kuwa SUE, JOHN na DONA wameuwawa kwa kuchomwa visu sehemu mbalimbali miilini mwao pia alama za kupigwa nyundo zimeonekana miilini mwao ina maana wauaji walikuwa wakiwaponda na nyundo pia ili wateseke zaidi.

FBI walikuwa na kazi ya kutambua wauaji, chanzo cha marehemu kutendewa hivyo, TINA yuko wapi maana ni ametekwa hapo, hii ilikuwa kesi ngumu maana ilikuwa haonekani mtuhumiwa ni nani na FBI walikuwa wakifanya kazi kwa kushirikiana na mapolisi wa KEDDIE.

FBI na mapolisi wa KEDDIE wakiendelea na uchunguzi wakagundua mwanakijiji mmoja alihama kijijini hapo baada ya mauaji na kuleta utata kuokana na uhamaji wake na alihamia himaya nyingine ya OREGON.

FBI waliwasiliana na maafisa wenzao kuhusu huyo mwanaume na kukamatwa kwaajili ya mahojiano na alifanikiwa kufaulu kipimo maalumu kitumikacho kwenye mahojiano kiitwacho LIE DETECTOR TEST au POLYGRAPH TEST na kuonekana hana uhusika wowote na mauaji ni alihama kikawaida tu.

LIE DETECTOR TEST ni kifaa au taratibu zinazopima na kurekodi viashiria vya kisaikolojia  vya presha ya damu, mapigo ya moyo, mwenendo wa ngozi wakati mtuhumiwa anahojiwa maswali ya mtego na wapelelezi ili kujua uhusika wake katika kesi aliyoshtumiwa.

Kifaa au taratibu hizi hutumiwa sana na mashirika ya CIA na FBI katika chunguzi zao na inakadiriwa hutoa ukweli kwa asilimia 90 maana mtuhumiwa anapohojiwa hivyo viashiria vitatu vya kisaikolojia lazima vitoe majibu na wapelelezi ndo wanahitimisha jawabu.

Wakati FBI wanamalizana na huyo mwanaume aliyehamia OREGON wanapata taarifa kutoka kwa afande mkuu KEDDIE bwana THOMAS kuwa kuna mwanamke mmoja aitwaye MARYLYN SMARTT amekuja kutoa taarifa kituoni hapo kuwa haoni nyundo nyumbani kwake na anadai hiyo nyundo inafanana na hiyo iliyokutwa eneo la mauaji.

Hiyo picha hapo juu ni mtu akiwa kwenye hicho kifaa Cha LIE DETECTOR TEST...!!!!

INAENDELEA....!!!!
Continue reading

MAUAJI NDANI YA KIJIJI CJA KEDDIE

SEHEMU YA SITA

Kuzunguka walianza na dirisha la chumba cha wasichana ambako ndo analala SHEILA na TINA na hawakumkuta TINA SHARP ila waliona matone ya damu kwenye kitanda hicho na sakafuni chini na kuelekea dirisha la chumba cha watoto wa kiume.

Kufika dirishani hapo wakashangaa kukuta RICK, GREG na rafiki yao JUSTIN bado wamelala zao na wanaonekana ni wazima ikabidi bwana SEABOLT kutegua mlango wa nyuma ambao uaelekea moja kwa moja kwenye chumba cha watoto wa kiume.

Bwana SEABOLT akawatoa watoto wote watatu ambao walionekana hawajui lolote na kuwapitisha mlango huo wa nyuma ili wasione ukatili wa ndugu zao na kuwaharibu kisaikolojia watoto na simu kituoni polisi ilishapigwa na mkewe.

Polisi wa kwanza kufika eneo la tukio alikuwa ni afande msaidizi kijijini KEDDIE aitwaye HANK CLEMENT ambaye ndo akaanzisha uchunguzi wa mauaji haya na kuangalia vizuri miili ya SUE, JOHN na DONA akagundua wamepitia vifo vikatili sana.

Kwanza marehemu wote walikuwa wamefungwa waya mikononi na miguuni na ile “medical tape” mdomoni ili sauti zao zisipae wakati wanakula mateso na ilionekana SUE alivyofungwa mdomoni bado sauti yake ilikuwa ikitoka au ilichanika maana kipande cha “medical tape” yake kiko chini na kuwekewa chupi yake mdomoni huku akiwa nusu uchi.

Marehemu wote wametolewa makoromeo nje na kisu bado kwenye sehemu mbalimbali miilini mwao kumechomwa visu mbalimbali na wauaji wao waliona haitoshi pia walikuwa wakiwaponda na nyundo sehemu mbalimbali na usulubiaji wa nyundo unaonekana pia miilini mwao.

Sababu miili imekutwa sebuleni na damu nyingi imemwagika sebuleni ikaonekana zoezi la utesaji na kuua lilifanyika hapo sebuleni na muuaji hakuwa mmoja ni lazima walianzia wawili, afande HANK anasema miili hiyo ilikuwa haingaliki mara mbili ni utesaji na uuaji wa kinyama sana ambao kijiji cha KEDDIE haujawahi kupitia.

Afande HANK akawahoji pia watoto wote kuhusu sakata la mauaji nyumbani hapo na watoto walionesha kutojua wala kusikia lolote usiku huo na kunyima mwanga upelelezi na kushangaa pia kwanini wauaji hao waliamua kuwaacha watoto hao watatu salama.

Maafande wengine nao wakawasili eneo la tukio na ilipita lisaa limoja mapolisi kugundua mwanafamilia mmoja aitwaye TINA SHARP hayupo ndani ya nyumba wakati alirudi na kulala humo ikabidi waanze kufuatilia maeneo ya karibu na hapo ukizingatia kijiji cha KEDDIE kimezungukwa na miti mirefu inayopelekea kuwa na msitu.

Utafutwaji wa mwanzo haukuzaa lolote kwa kushindwa kumpata TINA SHARP na kutojua kama yuko hai amaa laa ila walihesabia kama utekaji umefanyika dhidi ya TINA na yale matone ya damu kwenye kitanda na sakafun yaliwapa wasiwasi zaidi na hayakuendelea yale matone ila walijua yatakuwa ni ya TINA SHARP.

Hizo picha hapo juu ni eneo la tukio na huyo ambaye yuko nusu uchi ni SUE SHARP...!!!!

INAENDELEA....!!!!
Continue reading

MAUAJI NDANI YA KIJIJI CHA KEDDIE

SEHEMU YA TANO

Huku kwa familia ya SEABOLT mtoto TINA SHARP muda wa kuondoka ukawa umewadia na ilikuwa mida ya saa tatu na nusu usiku kuelekea saa nne usiku na hakusindikizwa na dada yake SHEILA SHARP kwasababu ya kujisahau na mambo ya luninga.

Bwana na bibi SEABOLT ndo walimsindikiza  kuhakikisha ameingia ndani kwao na kurudi nyumbani kwao ambako hapakukaa muda sana watoto wao pamoja na SHEILA SHARP nao wakaenda kulala na wa mwisho wakawa bwana na bibi SEABOLT.

Usiku mwingi kuingia wakati bwana na bibi SEABOLT wanaimarisha ndoa wakasikia sauti wasiyoielewa kama inaugulia uchungu, kuomba msaada, kulalamika,  yani haieleweki na sababu walikuwa dunia nyingine ya maraha ndo kabisa sauti hiyo ilikuwa ngumu kuitambua vizuri ila ilikuwa ikiwakera.

Bwana na bibi SEABOLT wakaamka kufuatilia sauti hiyo na walipitia chumba cha watoto kwa kuwakuta wanakoroma na wakaenda nje kusikilizia sauti hiyo kwa dakika kadhaa na kuona kimya gafla wanaona vijana wawili wanarudi na haraka wakawatambua ni JOHN SHARP na rafiki yake.

Basi wakajua sauti ile ni ya hao vijana na kuamua kurudi zao kulala kuendelea na kuimarisha ndoa, asubuhi kukakuchwa  na SHEILA SHARP akawahi kuamka kurudi nyumbani ili amsaidie mama yake kazi za asubuhi kama dada mkubwa.

Asubuhi hiyo ilikuwa saa moja na alivyokuwa akifungua mlango ili aingie ndani akaona kama mzito kidogo kwenye kuusukuma na kuongeza nguvu kidogo kuusukuma na kuweza kuingia ndani ambako ni sebuleni kwao.

SHEILA SHARP alipiga ukunga mmoja mkubwa sana na kukimbia kurudi kwakina familia ya SEABOLT ambao walishtushwa na jazba yake ambayo ilimchelewesha kujielezea nini kimemkimbiza haraka huko huku akilia na kuonekana mwenye uwoga uliopitiliza.

Familia ya SEABOLT ikafuata ishara zake kwa SHEILA SHARP kuwaonyeshea nyumbani kwao na kufika wakafungua mlango na kujionea nini kilichomgandisha SHEILA SHARP hata kuongea ashindwe ni kulikuwa kumetapakaa damu utazani sebule hiyo ni sehemu ya machinjio.

Hapo sebuleni walikuta miili ya SUE SHARP [mama], JOHN SHARP na DONA WINGATE ikiwa katika hali ya kinyama huku pembeni yao kukiwa na nyundo ambayo imelowa damu, visu viwili vimelowa damu kimojawapo ni kisu cha kawaida cha jikoni na kingine ni kisu cha buchani, waya na mkanda wa matibabu unaotumika mahospitalini [medical tape].

Familia ya SEABOLT ikaona isije ikaharibu uchunguzi wapelelezi watakapofika kwa kuishia mlangoni ila wakakumbuka humo ndani kwa msaada wa SHEILA SHARP kuwa kuna wadogo zake wengine na kubidi kuzunguka madirishani mwao kuwachungulia kujua hali zao halafu ndo watajua nini watafanya.

INAENDELEA....!!!!
Continue reading

MAUAJI NDANI YA KIJIJI CHA KEDDIE

SEHEMU YA NNE

Bwana SMARTT ili kuondokana na hali ya ugonjwa wa PTSD basi hupendwa sana kunywa pombe, mchana huo rafiki yake JOHN SHARP aitwaye DANA HALL WINGATE akaja kumpitia mwenzake waelekee mjini QUINCY ambako ni kilomita 8 kutoka KEDDIE.

JOHN SHARP akaomba ruhusa na kuruhusiwa na haikupita muda mtoto wake TINA naye akaomba ruhusa kwenda katika familia ya SEABOLT kuangalia luninga na kuruhusiwa na wakati huo tayari ameshakula na kuoga kabisa.

SHEILA akawa amebaki na mama yake kwa kutotoka kwenda sehemu yoyote siku nzima na ilipofika saa moja na nusu jioni na kuona JOHN SHARP hajarudi akamwambia SHEILA SHARP kuwa ajiandae waende mjini QUINCY kuwachukua wakina JOHN sababu walivyoaga walimuelekeza wamelekea sehemu gani hasa.

SHEILA na mama yake wakaondoka zao na kufika mahala walipo wakina JOHN SHARP kweli wakawakuta na kuwaambia muda wa kurudi nyumbani na vijana hawa walikuwa wamenuna sababu walipanga kuwapitia marafiki zao wengine waelekea kwenye sherehe.

Wote wanne wakarudi mpaka nyumbani sababu DANA HALL WINGATE alishapanga atalala kwakina JOHN SHARP, akili za watoto hawa bado zilikuwa  kwenye sherehe na chumba cha JOHN kilikuwa ni cha chini ya ardhi ukishaingia ndani unashuka chini.

Kufika mida ya saa tatu usiku SHEILA akamuomba mama yake aende kwakina familia ya SEABOLT aliko mdogo wake TINA akaangalie luninga na atalala huko huko na mama yake akamruhusu na kumkumbusha ahakikishe anamrudisha TINA SHARP nyumbani sababu usiku unayoyoma.

TINA kuondoka kuelekea kwa familia ya SEABOLT mama yake akaingia chumbani kumbe chumba cha chini waliko wakina JOHN SHARP walikuwa wakimvizia mama aingie chumbani waondoke zao kurudi mjini QUINCY ili wajumuike na marafiki zao kwenye sherehe.

Vijana hawa taratibu wakatoroka kwa kupitia mlango wa nyuma ili wakwepe dirisha la chumba cha mama yao asije akaaona bahati mbaya na faida iliyokuwepo ni mama yao sio mtu wa kufuatilia vyumbani mwao hasa kwa JOHN SHARP ambako ni chini [basement] na anawaamini sana watoto wake na kuwapenda sana.

JOHN na mwenzie wakaelekea barabara kuu na sababu ilikuwa ni usiku usafiri ni shida na wakaanza kupungia mkono magari yaliyokuwa yakipita ili kuomba lifti na kwa mida hiyo ya usiku gari zinapita moja moja ila kwa bahati nzuri wakabahatisha gari kwa kusimama kuwasikiliza shida yao.

Gari hiyo iliyosimama kulikuwepo na mtu mmoja mwanamke aitwaye DONNA WILLIAMS na kuwapa lifti vijana hao mpaka kwa marafiki zao ambao ndo wataungana nao kwenda kwenye sherehe na ilipangwa kufanyika OAKLAND CAMP.

INAENDELEA....!!!!
Continue reading

MAUAJI NDANI YA KIJIJI CHA KEDDIE

SEHEMU YA TATU

Familia ya SHARP ikahamia rasmi KEDDIE nyumba namba 28 na maisha mapya kuanza ingawa ilikuwa changamoto kwa familia hii kwasababu huko walikotoka mwanzo maisha yalikuwa mazuri kushinda wanapoenda kuhamia kwa kukosekana vitu kama luninga ambayo kwa watoto ni muhimu sana.

Maisha ya kijijini KEDDIE yalikuwa ya ujamaa fulani kwa wakazi wake kushirikiana sana katika mambo tofauti na usalama ulikuwa mkubwa ambao ulipelekea kuwepo kituo kimoja cha polisi ambacho hakikuwa na polisi zaidi ya watatu.

SIKU YA MAUAJI

Familia ya SHARP zima ilipokelewa vizuri kijijini KEDDIE kwa kupendwa sana na majirani na kupelekea watoto wa majirani kuja kushinda, kula na kulala nyumbani kwakina SHARP na wao wakina SHARP kwenda kwa majirani zao kushinda, kula na kulala.

Kama ilivyo desturi yao hiyo ya kushinda, kula na kulala siku moja ambayo ni tarehe 11 aprili 1981 ilianza vizuri bila kutegemewa kama ingekuja kuisha vibaya na kubaki kumbukumbu mbaya katika historia ya familia hii na Kijiji cha KEDDIE.

Mchana wa aprili 11 watoto wa mwisho wa SUE SHARP ambao ni RICKY na GREG SHARP walimuomba mama yao kuwa washinde na kulala na rafiki yako aitwaye JUSTIN EASON ambaye anatoka kwenye familia ya SMARTTS.

Famili ya SMARTTS inakaa nyumba namba 26 ikimaanisha ni majirani wa karibu tu na desturi yao ya kuruhusu watoto kushinda, kula na kulala ikachukua mkondo wake kwa SUE SHARP kukubali ila lazima amtaarifu kwanza mama yake JUSTIN EASON.

Sababu wanapoishi ni majirani SUE SHARP akamtaarifu mama yake JUSTINE EASON aitwaye MARILYN SMARTT kuwa watoto wake wanataka wabaki na JUSTIN EASON mpaka kesho ndo atarudi nyumbani na MARILYN SMARTT akaona sawa tena bora zaidi maana anamuona mtoto wake anakuwa na raha sana akiwa huko kuliko hapo nyubani kwake.

MARIYLYN alisema hivyo kwasababu mumewe MARTIN SMARTT ni baba wa kambo wa JUSTIN EASON na ni mtu fulani mkali sana sababu ya kuathirika kisaikolojia na vita ya VIETNAM na kumpelekea ugonjwa wa PTSD.

Ugonjwa wa PTSD ni hali isiyoisha inayomkumba mtu kwa kushindwa kupona au kusahau tukio au matukio ya kutisha aliyoshuhudia kwa macho yake, hali hii isipopata tiba inaweza kuishi milele na kumnyima raha mtu kama vile kustuka kustuka n.k

Vita ya VIETNAM inatajwa kama vita mbaya sana kwa taifa la MAREKANI ukizingatia ni vita waliyoshindwa vibaya sana sema wanatumia propaganda kama filamu kudanganya ukweli wa vita hiyo na wanajeshi wengi waliopigana wanasubuliwa sana na PTSD kutokana na kushuhudia ukatili na unyama mkubwa katika vita hiyo.

Hiyo picha hapo juu ni mtaa wanaokaa familia ya SHARP unaweza kuona nyumba yao namba 28 na za majirani zao....!!!!

INAENDELEA.....!!!!!
Continue reading

MAUAJI NDANI YA KIJIJI CHA KEDDIE

SEHEMU YA PILI

Kama kawaida kwenye nyumba zenye luninga lazima uhakikishe umeoga ndo uende usije ukachafua sebule ya watu na hivyo ndivyo wamiliki wa luninga wako na masharti yao, kufika saa mbili usiku SHEILA SHARP ambaye ni dada wa damu wa TINA LYNN SHARP naye alikuja kwa jirani yao huyo.

Kwahiyo wakawa ndugu wawili wanaangalia luninga na watoto wa familia ya SEABOLT na wakati SHEILA SHARP anakuja tayari alimuaga mama yake kuwa hatorudi nyumbani ni ataangalia luninga na kulala huko na mama mtu alimruhusu sababu anawaamini sana familia ya SEABOLT na ni familia rafiki na majirani wa karibu sana.

TINA LYNN SHARP hakuaga kama atalala naye huko kwa jirani kwahiyo usiku ilivyokuwa unayoyoma dada yake SHEILA akamtaka arudi nyumbani na kufika saa tatu na nusu mdogo wake akarudi nyumbani kwa kusindikizwa na bwana na bibi SEABOLT sababu watoto hawataki kubanduka kwenye luninga wamsindikize mwenzao.

Kuingia usiku mwingi SHEILA SHARP na rafiki zake wakiwa wameshalala bwana na bibi SEABOLT wakasikia sauti ambayo hawaielewi ila ikawa kama inawekera na kuwakata utamu wao maana walikuwa wanaimarisha ndoa na kuamua kuamka kwenda nje ya nyumba yao kusikiliza hiyo sauti inatokea wapi.

Wanandoa hawa kabla hawajatoka nje wakachungulia chumbani mwa watoto na kuona watoto wote wapo kamili pamoja na SHEILA SHARP na wanakoroma zao halafu wakatoka nje sasa ambako kulikuwa na giza tororo  na kusimama dakika kadhaa kusikilizia ile sauti liyokuwa ikiwasumbua wakiwa ndani wanakulana uroda inatokea wapi, turudi nyuma kidogo kujua chimbuko la sauti hii iliyowatoa wanandoa hawa chumbani mwao.

Mwezi disemba 1980 bibie GLENA SUSAN “SUE” SHARP alifanikiwa kuhitimisha uhusiano wake wa kindoa na mumewe JAMES SHARP baada ya kupata talaka yake na moja ya makubaliano waliyoingia ilkuwa ni watoto wakae na mama yao sababu walikuwa bado wadogo kiumri.

Mwanzoni familia hii ya SHARP kabla hawajaachana walikuwa wakiishi himayani CONNECTICUT na ili awe mbali na kumbukumbu za mahusiano yao akaamua yeye na familia yake wahame himayani hapo kwa kuhamia himayani CALIFORINA.

Wazo la kuhamia himayani CALIFORNIA lilikuja sababu kaka yake GLENA SUSAN SHARP anaishi CALIFORNIA na kumsihi ni sehemu nzuri ya kumsahaulisha mambo yote ya zamani na mumewe kwa kuanza maisha mapya na watoto wake.

GLENA SUSAN SHARP akiwa na watoto wake watano ambao ni JOHN SHARP mwenye umri wa miaka 15 [mototo mkubwa]. SHEILA SHARP mwenye umri wa miaka 14, TINA LYNN SHARP mwenye umri wa miaka 12, RICK mwenye umri wa miaka 10 na GREG SHARP mwenye umri wa miaka 5 walianza safari ya maisha mapya kwa kuhamia CALIFORNIA.

Kufika CALIFORNIA wakafikia kwa kaka[mjomba] yake aitwaye DONA na SUE akawa anashughulikia suala la kuhamia kwake na watoto na haikupita hata wiki akapata nyumba namba 28 kijijini KEDDIE na kununua vitu muhimu ili familia ihamie.

Hiyo picha hapo juu ni familia ya SHARP Ila picha ni ya kizamani wakiwa wadogo...!!!

INAENDELEA....!!!!
Continue reading

MAUAJI NDANI YA KIJIJI CHA KEDDIE

SEHEMU YA KWANZA

Hii ni makala inayoongelea kisa kimoja cha kusikitisha na kusisimua sana kilichotokea nchini MAREKANI katika himaya ya CALIFORNIA kijijini KEDDIE ambako kulifanyika mauaji ya kikatili sana uisyotegema mwandamu anaweza kumfanyia mwanadamu mwenzie.

Kuna muda unajiuliza hawa binadamu wenye roho mbaya hivi wanazaliwa na binadamu kweli maana ule utu haupo kabisa ni unyama juu ya unyama na kujiona kama vile huna dhambi ukijilinnganisha na wanadamu wanaotenda huo unyama.

Hofu ya Mungu imepotea mioyono mwao ni kujawa na roho za kishetani katika kutimiza haja zao za kibinadamu kwa kuwapitisha wenzao kwenye mateso makali ya kikatili na kurudi kwenye msemo wa kufa sio tatizo ila tatizo ni unakufaje.

Sasa hawa wakatili walihakikisha binadamu wenzao wanapita mateso makali ya hali ya juu mpaka pale roho inapotoka na watendaji hawa wakatili wanakuwa sio watu wa kawaida ni wana uledi mkubwa wa kupanga matukio ya kikatili ili kuhakikisha wapelelezi hawali mshahara wa bure ni wanautumikia vizuri.

Kodi za wananchi zinatumika vizuri, polisi walianza uchunguzi wa awali na kuona hapana hii sio kesi ya kupambana na wao na kuja wazee wa hizo kazi FBI ambao wanajulikana ubora wao wanapokuwa kazini ili kuhakikisha wakatili wote wanatiwa nguvuni na sheria kuchukua mkondo wake.

Ukiangalia kwa wasiwasi kama vile kesi rahisi na ndicho hata FBI walichoona kwa kuona wapelelezi wa kipolisi wanagwaya kesi nyepesi kama hiyo ila nao kuingia kupambana na kesi hii wakaona hapana ngoja waingie wazima wazima na kupambana nayo usiku na mchana.

Moja ya kesi ngumu kuwahi kuwafikia FBI mezani kwao na huku nje raia na vyombo vya habari hawako mbali ni wanawanusa nyuma FBI kujua kila hatua wanayofikia na kuwapa presha huku wenyewe wakijinasibu ni kesi nyepesi kwao.

Kijiji cha KEDDIE chenyewe kidogo hakina matukio ya kikatili kama hili na wanajuana wote kwasababu wako wachache ila wanakuja kuharibiwa hali ya hewa na mauaji haya na kufanya ulinzi na usalama kuongezwa kijiji hapo ambako hata wagambo kulikuwa hakunaga.

KABLA YA MAUAJI

Tarehe 11 aprili 1981 binti mmoja ajulikanae kama TINA LYNN SHARP ambaye amezaliwa tarehe 22 julai 1968 ina maana kwa wakati huo alikuwa na umri wa miaka 12 alikuwa kwa nyumba/kijumba/kibanda [CABIN] ya jirani yake namba 27.

Kijijini KEDDIE nyumba zao zina namba kwa kufuatana na binti TINA LYNN SHARP alikuwa jirani nyumba namba 27 na kwao ni nyumba namba 28 maana yake ni majirani wa karibu sana na ni tabia ya binti huyu na ndugu zake kwenda kwa jirani yao kukodolea macho luninga hasa huyo TINA LYNN SHARP ndo anapenda Sana luninga. 

Hiyo picha hapo juu ni ndo nyumba ya kina TINA LYNN SHARP (CABIN 28)...!!!!

INAENDELEA....!!!!
Continue reading