Tuesday, January 7, 2020

MAUAJI NDANI YA KIJIJI CHA KEDDIE

SEHEMU YA TANO

Huku kwa familia ya SEABOLT mtoto TINA SHARP muda wa kuondoka ukawa umewadia na ilikuwa mida ya saa tatu na nusu usiku kuelekea saa nne usiku na hakusindikizwa na dada yake SHEILA SHARP kwasababu ya kujisahau na mambo ya luninga.

Bwana na bibi SEABOLT ndo walimsindikiza  kuhakikisha ameingia ndani kwao na kurudi nyumbani kwao ambako hapakukaa muda sana watoto wao pamoja na SHEILA SHARP nao wakaenda kulala na wa mwisho wakawa bwana na bibi SEABOLT.

Usiku mwingi kuingia wakati bwana na bibi SEABOLT wanaimarisha ndoa wakasikia sauti wasiyoielewa kama inaugulia uchungu, kuomba msaada, kulalamika,  yani haieleweki na sababu walikuwa dunia nyingine ya maraha ndo kabisa sauti hiyo ilikuwa ngumu kuitambua vizuri ila ilikuwa ikiwakera.

Bwana na bibi SEABOLT wakaamka kufuatilia sauti hiyo na walipitia chumba cha watoto kwa kuwakuta wanakoroma na wakaenda nje kusikilizia sauti hiyo kwa dakika kadhaa na kuona kimya gafla wanaona vijana wawili wanarudi na haraka wakawatambua ni JOHN SHARP na rafiki yake.

Basi wakajua sauti ile ni ya hao vijana na kuamua kurudi zao kulala kuendelea na kuimarisha ndoa, asubuhi kukakuchwa  na SHEILA SHARP akawahi kuamka kurudi nyumbani ili amsaidie mama yake kazi za asubuhi kama dada mkubwa.

Asubuhi hiyo ilikuwa saa moja na alivyokuwa akifungua mlango ili aingie ndani akaona kama mzito kidogo kwenye kuusukuma na kuongeza nguvu kidogo kuusukuma na kuweza kuingia ndani ambako ni sebuleni kwao.

SHEILA SHARP alipiga ukunga mmoja mkubwa sana na kukimbia kurudi kwakina familia ya SEABOLT ambao walishtushwa na jazba yake ambayo ilimchelewesha kujielezea nini kimemkimbiza haraka huko huku akilia na kuonekana mwenye uwoga uliopitiliza.

Familia ya SEABOLT ikafuata ishara zake kwa SHEILA SHARP kuwaonyeshea nyumbani kwao na kufika wakafungua mlango na kujionea nini kilichomgandisha SHEILA SHARP hata kuongea ashindwe ni kulikuwa kumetapakaa damu utazani sebule hiyo ni sehemu ya machinjio.

Hapo sebuleni walikuta miili ya SUE SHARP [mama], JOHN SHARP na DONA WINGATE ikiwa katika hali ya kinyama huku pembeni yao kukiwa na nyundo ambayo imelowa damu, visu viwili vimelowa damu kimojawapo ni kisu cha kawaida cha jikoni na kingine ni kisu cha buchani, waya na mkanda wa matibabu unaotumika mahospitalini [medical tape].

Familia ya SEABOLT ikaona isije ikaharibu uchunguzi wapelelezi watakapofika kwa kuishia mlangoni ila wakakumbuka humo ndani kwa msaada wa SHEILA SHARP kuwa kuna wadogo zake wengine na kubidi kuzunguka madirishani mwao kuwachungulia kujua hali zao halafu ndo watajua nini watafanya.

INAENDELEA....!!!!
Previous Post
Next Post

0 Comments: