SEHEMU YA 11
Huo ulikuwa ushahidi wa JUSTIN EASON kwa FBI na baada ya mchoro kukamilika alioneshwa hizo picha zilivyotoka na kusema wanafanana na huo mchoro na FBI wakautumia huo mchoro wa picha kwenye chunguzi zao kama watabahatika kumpata mtu anayefanana na huo mchoro.
Ushuhuda alioongea JUSTINE EASON hauaminiki asilimi 100 kwasababu mara kwanza alikataa kuwa hakusikia lolote ila safari hiyo amekubali na kuelezea hivyo ila mwisho wa siku FBI mchoro wa hao wauaji haukuwasaidia kwani hawakupata mtu anayefanana na hao.
FBI wakaendelea kinyonge na pelelezi zao huku wakiwa hawana mwanga wa mauaji ya familia ya SHARP wala kumpata TINA SHARP, kuingia mwaka 1984 tarehe 22 aprili muokota makopo mmoja katika kaunti ya BUTTE aliokota kipande cha fuvu.
Muokota makopo huyu akaamua kukipeleka hicho kipande cha fuvu polisi na mkuu wa polisi kaunti ya BUTTE alitangaza kwa vyombo vya habari kuwa kumeokotwa kipande cha fuvu na uchunguzi wake unafanyika kujua ni fuvu la binadamu au mnyama ili hatu zingine ziendelee ila kimuonekana ni fuvu la binadamu sema lazima wachunguzi wa kitabibu wathibitishe hilo.
Wakati tangazo hili limesambaa kote mkuu huyu wa polisi akapigiwa simu na mtu asiyemjua na kumwambia kuwa kipande hicho fuvu ni cha mtoto mmoja aitwaye TINA SHARP wa kijijini KEDDIE na kuendelea kuongea kuwa eneo hilo lina mabaki mengine ya TINA SHARP na simu ikakatwa..
Mkuu wa polisi alishangazwa na simu hiyo na kumbukumbu ya kesi hiyo ikamjia kwasababu ilikuwa habari ya nchi kwa kila mmoja kuongelea na kufuatilia kesi hiyo na haraka akawasiliana na FBI ili kuwalelezea kuhusu ujumbe wa simu hiyo.
FBI haraka wakafika na kuelekea eneo kulikookotwa fuvu na ukaguzi ukaanza mara moja na kweli baada ya ukaguzi walifanikiwa kupata mabaki mengine ya binadamu pamoja na blanketi, jaketi na suruali ambavyo ni mali za TINA.
FBI wakafikisha mabaki hayo pamoja na lile fuvu kwa wachunguzi wa kitabibu na kuwataka kukimbiza uchunguzi kama vinahusiana na TINA na baada ya uchunguzi matokeo yakatoka na kuonesha mabaki hayo yote ni ya TINA SHARP.
Mabaki hayo yalifikikaje, nani aliyaleta, alikufaje inabaki kitendawili kwa wapelelezi na kutoka hapo mabaki yalipokutwa mpaka Kijiji KEDDIE ni umbali wa kilomita 160 kwahiyo ni safari mtoto TINA alipelekwa kuuwawa huko.
Wapelelezi walikuwa wakijiuliza maswali magumu ni kwanini TINA SHARP apelekwe kuuwawa mbali tofauti na wenzie au ubakaji ulifanyika kwanza kabla ya mauaji yote bado ni maswali magumu na FBI wakarudia kufuatilia ile simu iliyopigwa kwa mkuu wa polisi ili asaidie upelelezi Kama sio muhusika mmojawapo wa mauaji ya kijijini KEDDIE.
Hiyo picha hapo juu ni mchoro wa hao wanaume kwa maelezo kutoka kwa mtoto JUSTIN...!!!!!
INAENDELEA....!!!!!
0 Comments: