SEHEMU YA KWANZA
Hii ni makala inayoongelea kisa kimoja cha kusikitisha na kusisimua sana kilichotokea nchini MAREKANI katika himaya ya CALIFORNIA kijijini KEDDIE ambako kulifanyika mauaji ya kikatili sana uisyotegema mwandamu anaweza kumfanyia mwanadamu mwenzie.
Kuna muda unajiuliza hawa binadamu wenye roho mbaya hivi wanazaliwa na binadamu kweli maana ule utu haupo kabisa ni unyama juu ya unyama na kujiona kama vile huna dhambi ukijilinnganisha na wanadamu wanaotenda huo unyama.
Hofu ya Mungu imepotea mioyono mwao ni kujawa na roho za kishetani katika kutimiza haja zao za kibinadamu kwa kuwapitisha wenzao kwenye mateso makali ya kikatili na kurudi kwenye msemo wa kufa sio tatizo ila tatizo ni unakufaje.
Sasa hawa wakatili walihakikisha binadamu wenzao wanapita mateso makali ya hali ya juu mpaka pale roho inapotoka na watendaji hawa wakatili wanakuwa sio watu wa kawaida ni wana uledi mkubwa wa kupanga matukio ya kikatili ili kuhakikisha wapelelezi hawali mshahara wa bure ni wanautumikia vizuri.
Kodi za wananchi zinatumika vizuri, polisi walianza uchunguzi wa awali na kuona hapana hii sio kesi ya kupambana na wao na kuja wazee wa hizo kazi FBI ambao wanajulikana ubora wao wanapokuwa kazini ili kuhakikisha wakatili wote wanatiwa nguvuni na sheria kuchukua mkondo wake.
Ukiangalia kwa wasiwasi kama vile kesi rahisi na ndicho hata FBI walichoona kwa kuona wapelelezi wa kipolisi wanagwaya kesi nyepesi kama hiyo ila nao kuingia kupambana na kesi hii wakaona hapana ngoja waingie wazima wazima na kupambana nayo usiku na mchana.
Moja ya kesi ngumu kuwahi kuwafikia FBI mezani kwao na huku nje raia na vyombo vya habari hawako mbali ni wanawanusa nyuma FBI kujua kila hatua wanayofikia na kuwapa presha huku wenyewe wakijinasibu ni kesi nyepesi kwao.
Kijiji cha KEDDIE chenyewe kidogo hakina matukio ya kikatili kama hili na wanajuana wote kwasababu wako wachache ila wanakuja kuharibiwa hali ya hewa na mauaji haya na kufanya ulinzi na usalama kuongezwa kijiji hapo ambako hata wagambo kulikuwa hakunaga.
KABLA YA MAUAJI
Tarehe 11 aprili 1981 binti mmoja ajulikanae kama TINA LYNN SHARP ambaye amezaliwa tarehe 22 julai 1968 ina maana kwa wakati huo alikuwa na umri wa miaka 12 alikuwa kwa nyumba/kijumba/kibanda [CABIN] ya jirani yake namba 27.
Kijijini KEDDIE nyumba zao zina namba kwa kufuatana na binti TINA LYNN SHARP alikuwa jirani nyumba namba 27 na kwao ni nyumba namba 28 maana yake ni majirani wa karibu sana na ni tabia ya binti huyu na ndugu zake kwenda kwa jirani yao kukodolea macho luninga hasa huyo TINA LYNN SHARP ndo anapenda Sana luninga.
Hiyo picha hapo juu ni ndo nyumba ya kina TINA LYNN SHARP (CABIN 28)...!!!!
INAENDELEA....!!!!
0 Comments: