SEHEMU YA SABA
Majirani wa SHARP wakaanza kuhojiwa kama walisikia lolote na kila mmoja alisema kuwa hawakusikia lolote zaidi ya bwana na bibi SEABOLT ndo walisikia sauti isiyoeleweka wakajua ni za wale vijana ndo wanarudi kutoka kwenye sherehe kumbe yawezakana ndo sauti ilikuwa ikitoka nyumbani kwa SUE SHARP baada ya kuvamiwa na wauaji.
Sasa mapolisi wakawa wanajiuliza kama sauti iliweza kusikika mpaka kwa jirani SEABOLT na kuwakera imekuwaje watoto wameshindwa kuisikia ila wakapotezea na kingine kilishowangaza kwanini wauaji waliamua kuacha silaha zao za mauaji eneo le tukio ili iweje na kumchukua TINA SHARP kwasababu gani..? yote yakawa maswali magumu kwa wakati huo.
Afande mkuu kijijini KEDDIE aitwaye DOUG THOMAS ambaye naye alikuja eneo la tukio alipiga simu juu kuomba msaada wa kiuchunguzi zaidi kuhusu tukio la mauaji kijijini kwake na maafisa wa FBI wakatumwa kwenda kijijini KEDDIE kupambana na kesi hii.
FBI kufika kijijini KEDDIE walichukua ripoti za uchunguzi w awali kutoka kwa afande mkuu DOUG THOMAS ambazo zilikuwa zimeambatanishwa na ripoti za kitabibu baada ya miili ya kina SUE, JOHN na DONA kufikishwa hospitalini.
Ripoti ya kitabibu ilisema kuwa SUE, JOHN na DONA wameuwawa kwa kuchomwa visu sehemu mbalimbali miilini mwao pia alama za kupigwa nyundo zimeonekana miilini mwao ina maana wauaji walikuwa wakiwaponda na nyundo pia ili wateseke zaidi.
FBI walikuwa na kazi ya kutambua wauaji, chanzo cha marehemu kutendewa hivyo, TINA yuko wapi maana ni ametekwa hapo, hii ilikuwa kesi ngumu maana ilikuwa haonekani mtuhumiwa ni nani na FBI walikuwa wakifanya kazi kwa kushirikiana na mapolisi wa KEDDIE.
FBI na mapolisi wa KEDDIE wakiendelea na uchunguzi wakagundua mwanakijiji mmoja alihama kijijini hapo baada ya mauaji na kuleta utata kuokana na uhamaji wake na alihamia himaya nyingine ya OREGON.
FBI waliwasiliana na maafisa wenzao kuhusu huyo mwanaume na kukamatwa kwaajili ya mahojiano na alifanikiwa kufaulu kipimo maalumu kitumikacho kwenye mahojiano kiitwacho LIE DETECTOR TEST au POLYGRAPH TEST na kuonekana hana uhusika wowote na mauaji ni alihama kikawaida tu.
LIE DETECTOR TEST ni kifaa au taratibu zinazopima na kurekodi viashiria vya kisaikolojia vya presha ya damu, mapigo ya moyo, mwenendo wa ngozi wakati mtuhumiwa anahojiwa maswali ya mtego na wapelelezi ili kujua uhusika wake katika kesi aliyoshtumiwa.
Kifaa au taratibu hizi hutumiwa sana na mashirika ya CIA na FBI katika chunguzi zao na inakadiriwa hutoa ukweli kwa asilimia 90 maana mtuhumiwa anapohojiwa hivyo viashiria vitatu vya kisaikolojia lazima vitoe majibu na wapelelezi ndo wanahitimisha jawabu.
Wakati FBI wanamalizana na huyo mwanaume aliyehamia OREGON wanapata taarifa kutoka kwa afande mkuu KEDDIE bwana THOMAS kuwa kuna mwanamke mmoja aitwaye MARYLYN SMARTT amekuja kutoa taarifa kituoni hapo kuwa haoni nyundo nyumbani kwake na anadai hiyo nyundo inafanana na hiyo iliyokutwa eneo la mauaji.
Hiyo picha hapo juu ni mtu akiwa kwenye hicho kifaa Cha LIE DETECTOR TEST...!!!!
INAENDELEA....!!!!
0 Comments: