Tuesday, January 7, 2020

MAUAJI NDANI YA KIJIJI CHA KEDDIE

SEHEMU YA TATU

Familia ya SHARP ikahamia rasmi KEDDIE nyumba namba 28 na maisha mapya kuanza ingawa ilikuwa changamoto kwa familia hii kwasababu huko walikotoka mwanzo maisha yalikuwa mazuri kushinda wanapoenda kuhamia kwa kukosekana vitu kama luninga ambayo kwa watoto ni muhimu sana.

Maisha ya kijijini KEDDIE yalikuwa ya ujamaa fulani kwa wakazi wake kushirikiana sana katika mambo tofauti na usalama ulikuwa mkubwa ambao ulipelekea kuwepo kituo kimoja cha polisi ambacho hakikuwa na polisi zaidi ya watatu.

SIKU YA MAUAJI

Familia ya SHARP zima ilipokelewa vizuri kijijini KEDDIE kwa kupendwa sana na majirani na kupelekea watoto wa majirani kuja kushinda, kula na kulala nyumbani kwakina SHARP na wao wakina SHARP kwenda kwa majirani zao kushinda, kula na kulala.

Kama ilivyo desturi yao hiyo ya kushinda, kula na kulala siku moja ambayo ni tarehe 11 aprili 1981 ilianza vizuri bila kutegemewa kama ingekuja kuisha vibaya na kubaki kumbukumbu mbaya katika historia ya familia hii na Kijiji cha KEDDIE.

Mchana wa aprili 11 watoto wa mwisho wa SUE SHARP ambao ni RICKY na GREG SHARP walimuomba mama yao kuwa washinde na kulala na rafiki yako aitwaye JUSTIN EASON ambaye anatoka kwenye familia ya SMARTTS.

Famili ya SMARTTS inakaa nyumba namba 26 ikimaanisha ni majirani wa karibu tu na desturi yao ya kuruhusu watoto kushinda, kula na kulala ikachukua mkondo wake kwa SUE SHARP kukubali ila lazima amtaarifu kwanza mama yake JUSTIN EASON.

Sababu wanapoishi ni majirani SUE SHARP akamtaarifu mama yake JUSTINE EASON aitwaye MARILYN SMARTT kuwa watoto wake wanataka wabaki na JUSTIN EASON mpaka kesho ndo atarudi nyumbani na MARILYN SMARTT akaona sawa tena bora zaidi maana anamuona mtoto wake anakuwa na raha sana akiwa huko kuliko hapo nyubani kwake.

MARIYLYN alisema hivyo kwasababu mumewe MARTIN SMARTT ni baba wa kambo wa JUSTIN EASON na ni mtu fulani mkali sana sababu ya kuathirika kisaikolojia na vita ya VIETNAM na kumpelekea ugonjwa wa PTSD.

Ugonjwa wa PTSD ni hali isiyoisha inayomkumba mtu kwa kushindwa kupona au kusahau tukio au matukio ya kutisha aliyoshuhudia kwa macho yake, hali hii isipopata tiba inaweza kuishi milele na kumnyima raha mtu kama vile kustuka kustuka n.k

Vita ya VIETNAM inatajwa kama vita mbaya sana kwa taifa la MAREKANI ukizingatia ni vita waliyoshindwa vibaya sana sema wanatumia propaganda kama filamu kudanganya ukweli wa vita hiyo na wanajeshi wengi waliopigana wanasubuliwa sana na PTSD kutokana na kushuhudia ukatili na unyama mkubwa katika vita hiyo.

Hiyo picha hapo juu ni mtaa wanaokaa familia ya SHARP unaweza kuona nyumba yao namba 28 na za majirani zao....!!!!

INAENDELEA.....!!!!!
Previous Post
Next Post

0 Comments: