EPISODE 01
Majira ya saa nane za usiku msichana Suzana alikuwa akitoka kujirusha katika ukumbi wa Bilicanas. Kilichomshtua kilikuwa kutoweka kwa mpenzi wake Sammy ambaye aliondoka bila kumuaga. Wazo lake la kwanza lilikuwa Sammy kaondoka na msichana mwingine akijua kabisa yeye ndiye mchumba wake.Akiwa amekasirika kwa kitendo cha Sammy kuondoka na kumuacha peke yake, kila alipopiga simu yake iliita bila kupokelewa kitu kilichoonesha dharau. Aliamua kurudi nyumbani kwake japo alipanga siku ile
kulala kwa Sammy. Aliendesha gari akiwa amefura kwa hasira huku machozi yakimtoka kutokana kitendo alichotendewa na mpenzi wake ambaye ndiye aliyemtoa kitandani alipokuwa amekwisha kulala. Suzana awaliza mengi juu ya kitendo cha mpenzi wake kumwita klabu na kumkimbia.Wakati akitoka Bilicanas mvua ilianza kunyesha, hakutaka kuisubiri aliamua kwenda nayo ili awahi nyumbani angalau alale kwa muda mchache ili asubuhi awahi kanisani misa ya kwanza.Mvua ilikuwa kubwa iliyoambatana na upepo mkali kitu kilichomfanya ashindwe kuona mbele ilimbidi alisimamishe gari pembeni ya daraja ya Salenda ili kusubiri upepo upungue ndipo aendelee na safari yake. Upepo ule haukuchukua muda ulitulia na mvua ilikuwa imekatika.Alipowasha gari liligoma kuwaka, alirudia zaidi ya mara tano kuzungusha funguo lakini liligoma kuwaka. Kuteremka kwenye gari alishindwa kutokana na hali ya kiza cha kutisha nje. Wasi wasi ulimtawala na kujiuliza atatokaje pale au ndio atalala mpaka asubuhi.Hasira zilizidi kumpanda Suzana kutokana na kukimbiwa na mpenzi wake na kuharibikiwa na gari. Kutokana na hofu aliyokuwa nayo alihakikisha milango na vioo vyote vimefungwa vizuri. Alijikuta akipiga dua kumuomba Mungu amuokoe na janga lile kwa kupata msaada wa watu wenye gari kumsaidia kuwasha gari lake. Lakini kwa muda ule hakukuwa na dalili ya gari lolote kupita.Akiwa ameinama mikono ameikutanisha kifuani kwake alishtushwa na upepo makali uliovuka toka baharini na kulifanya gari lake kuyumba na kusogea kidogo. Kwa woga uliompata Suzana alijikuta akitokwa na haja ndogo bila kuelewa. Alitamani kulia lakini aliamini sauti yake haitasaidia lolote kwa vile hakukuwa na wakumsaidia.Aliinama kwa woga hakutaka kuangalia popote zaidi ya kusubiri chochote kitakachomtokea. Baada ya muda hali ile ilitulia, Suzana alinyanyua kichwa taratibu ili achukue simu ampigie baba yake amfuate eneo lile ambalo lilikuwa limemuweka katika hali ya hatari.Aliponyanyua uso achukue simu iliyokuwa kwenye kwenye dash board, alishtushwa na mwanga mkali kama jua la saa saba mchana. Aliangalia katikati ya bahari palipokuwa kunatoka mwanga ule. Alituliza macho baada ya kumuona mwanamke aliyekuwa amevaa gauni jeupe lilikuwa liking’aa kutokana na mapambo yake.Hali ile ilimfanya asahau yalitomtokea muda mfupi na kutuliza macho kumuangalia yule mwanamke aliyekuwa akitembea juu ya maji huku nyuma akisindikizwa na wasichana walikuwa wamebeba vikapu vidogo vilivyokuwa na maua ambayo walimwagia kila hatua ilivyopigwa huku wakiimba nyimbo nzuri.Suzana alijikuta akipata ujasiri wa ajabu kwa kufungua dirisha kidogo ili aweze kusikia watu wale walikuwa wakiimba kitu gani. Zilikuwa sauti nzuri kama za kaswida zilizoimbwa kwa lugha ya kiarabu. Nyimbo zile zilimvutia na kujikuta akiwa na hamu ya kuwaona watu wale waliokuwa wakitembea juu ya maji kwa mstari mbele huku akitangulia yule mwanamke ambaye usoni kwake kulikuwa kunawaka kama taa na kushindwa kuiona sura yake vizuri.Suzana alijikuta akisahau kama wale watu walikuwa wakitembea juu ya maji zaidi ya kushangazwa na sherehe ile ambayo toka azaliwe hajawahi kuona sherehe ya aina ile ya mtu mmoja kutangulia mbele wengine kumfuata nyuma huku wakimuwagia maua na kumwimbia nyimbo nzuri.Baada ya muda watu wote walikaa mstari mmoja, kisha yule mwanamke aliyekuwa amependeza kuliko wote alipita katikati yao na kupigiwa vilegele huku akitupiwa maua. Manukato ya maua yalisambaa mpaka ndani ya gari la Suzana alilokuwa amefungua kioo kidogo kusikia nyimbo alizokuwa anaimbiwa yule mwanamke ambaye alionekana kama bibi harusi lakini muda wote hakumuona bwana harusi wala mwanaume kwenye kundi lile.Yule mwanamke alipita kwenye mstari mpaka mwisho alitembea peke yake bila kufuatwa na mtu kisha aligeuka na kuwapungia mkono wenzake ambao nao walimpungia huku wakimrushia maua. Baada ya kutembea kidogo Suzana alimshuhudia yule mwanamke alikunja gauni lake usawa na kifua na kushangaa kumuona akitembea ndani ya maji yaliyokuwa yamemfika tumboni.Suzana alijikuta akishtuka na kujiuliza yupo ndotoni au anaona kweli, kilichomshangaza ni umbali aliotoka yule mwanamke akitembea juu ya maji. Lakini cha kushangaza alipokaribia ufukweni alionekana yupo ndani ya maji yaliyomfikia tumboni.Aliendelea kumtazama amuone anakwenda wapi, yule mwanamke baada ya kutoka ndani ya maji alitembea juu ya mchanga kulifuata lile gari. Kila hatua ilivyokuwa ikipigwq ilizidi kumtisha Suzana, alijikuta akimshangaa kutaka kuijua sura yake. Alituliza macho yake kwenye uso wa yule mwanamke aliyekuwa akiisogelea gari huku manukato makali yakizidi kujaa ndani ya gari.Kilichomshangaza zaidi ni sura ya yule mwanamke alikuwa akifanana naye kwa kila kitu umbile na sura. Suzana alishtuka na kufunga kioo haraka ili mtu yule ambaye yeye alimuona wa muujiza asiingie kwenye gari. Yule mwanamke alisogea kwenye gari na kuligusa, ajabu baada ya kuligusa lile gari alitoweka ghafla.Suzana akiwa anatetemeka alijaribu kuwasha gari kwa mara nyingine, ajabu ya Mungu gari liliwaka aliondoka eneo lile kwa mwendo wa kasi. Alipofika nyumbani kulikuwa kumekucha, alikwenda kuoga haraka ili awahi kanisani kwani muda ulikuwa umekwenda.Baada ya kuoga alirudi ndani, lakini alishtushwa na harufu ya manukato ambayo aliyasikia muda mfupi darajani gari lake lilipozima . Hakutaka kulifikiria sana jambolile kwani muda ulikuwa umekwenda, alikwenda kwenye kabati kubadili nguo ili awahi kanisani.Baada ya kumaliza kubadili nguo alijikuta akiingiwa na uvivu na kwenda kukaa kwenye kitanda, haikupita muda usingizi mzito ulimshika na kulala bila kujielewa, aliposhtuka usingizini alishtuka kuiona familia yake yote imesimama mbele yake. Alijiuliza kuna nini, alipojiangalia alijiona akiwa amevaa nguo za kuendea kanisani.“Suzana upo sawa?” Mama yake alimuuliza. “Mbona unaniuliza hivyo? Halafu mbona kama wote mlikuwa mnalia kuna nini mbona mnanitisha?
“Suzana,” mama yake alimwita tena akiwa bado anamshangaa.. “Abee mama.” “Upo sawa?” Mama yake alimuuliza huku akimkagua mwanaye kwa kumshika kila kona ya mwili. “Nipo sawa mama, kwani vipi?” “Siamini kweli Mungu wa ajabu.” “Mama mbona sikuelewi nilitokewa na nini?” Suzana alizidi kushangaa.
Je nini kilimtokea SUZANA? SHARE KWA WINGI ILI NIWE KARIBU NAWE KWENYE KILA HATUA YA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA.

0 Comments: