EPISODE : 04
ILIPOISHA
Nilipofika darasa la saba walimu wakawa wanahisi kuwa ni mjamzito, kwa kukata mzizi wa fitina siku moja wakatuchukua wasichana wote tuliovunja ungo na kutupeleka zahanati kupima ujauzito.
Mama yangu! si ndo nikagundulika nina ujauzito wa miezi mitatu mwenzenu! Tena ilikuwa bado mwezi mmoja tu tufanye mtihani wa kumaliza elimu ya msingi!
JIACHIE MWENYEWE...
Hata hivyo hamna noma sikukonda wala nini, kwa kuwa hata hiyo shule yenyewe sikuwa na lolote kila tukifanya mtihani nilikuwa wa kwanza kutoka mwisho !
Basi mwaya sikuweza tena kufanya mtihani, baada ya kufika miezi tisa nikajifungua lakini mtoto ikawa bahati mbaya akafa.
Baada ya kurejea vyema kwa afya yangu, mama mdogo yaani mke wa baba yangu mdogo ambaye alikuwa akiishi Dar alipokuja kijijini kwetu kututembelea akanitaka tuondoke wote kwani hakukuwa na nilichokuwa nafanya kule kijijini.
Nikaikubali mara moja ofa hiyo kwani hata mimi nilikuwa nimeshaanza kuyachoka maisha ya kijijini, kwanza watu walikuwa wananiuzi sana maana nilikuwa midomoni mwao kila kukicha.
Eti oo mtoto yule katoa mimba, mara kasaga mtoto mara ooo hajachezwa ngoma yaani watu wengine nyie wana mambo ya kizamani kweli kwani kuchezwa ngoma ndio nini?
Yaani bora hata wangekuwa wananisimanga kuhusu kukatisha masomo lakini wao wanaona kuchezwa ngoma ndio suala la maana.
Basi mwanya nikatumbukia jijini Dar es salam, mwanzoni nilionekana wa kawaida sana lakini baada ya kuanza kutumia vipodozi nikaanza kuwa tishio.
Unafikiri hata muda wa kuinjoi na masharo wa Dar niliupata!
Wakati wakianza kunisogelea si ndo likaja hilo zee la East Africa na kumwambia baba mdogo tena bila ya aibu kuwa linataka kunioa sambamba na kuleta misaada midogomidogo pale nyumbani, likijifanya lina mihela mpaka linaumwa.
Haki ya nani siku hiyo mama mdogo aliponiambia kuwa zee lile linataka kunioa nilichukia sana na nilimwambia wazi kuwa silitaki.
Lakini baba mdogo alipopeleka taarifa kwa baba kuwa kuna mwanaume anataka kunioa ila mimi nimekataa, baba akikuja juu na kuniambia ni lazima niolewe hasa alizidisha kunilazimisha aliposikia kuwa jianaume lenyewe ni zee lililopata mafao ya East Afrika ndio akazidi kuwa mkali.
Basi hilo zee likaanza kujipendekeza likawa linaenda hadi kule kijijini kwetu na kukaa hata wiki na likienda likawa linabeba mizawadi kibao kuanzia nyumbani hadi kwa vijana na wazee wa kijijini kwa kuwanunulia pombe kila mtu, kiasi cha kukubalika na kila mtu kule kijijini kwetu.
Likajifagilia si kidogo kiasi kwamba kila mtu akawa analaani aliposikia kuwa mimi natakiwa kuolewa na lile zee ila mimi sitaki.
Kutokana na shinikizo kubwa la wazazi, ndugu na wanakijiji basi nikaamua kulikubali zee hilo japo kwa shingo upande.
Ikafanyika harusi Bab kubwa na kama ningeolewa na kijana mwenzangu ambaye nimemuweka rohoni, siku hiyo ningefurahi sana lakini haikuwa hivyo.
Basi baada ya harusi hiyo ndipo nikaenda nyumbani kwa zee hilo kuanza maisha mapya. Nilipofika huko nako nilipigwa na butwaa!
Yaani mzee huyo ambaye kijijini kwetu akawa anatamba kuwa anataka kununua basi kama mbili ziwe zinapiga ruti kutoka kijijini kwetu kuja Dar kwakuwa ameona kuwa kuna adha ya usafiri, kwani tunachajiwa nauli ya Dar tu Moro wakati kwetu ni jirani tu na Chalinze.
Alijidai pia kuwa yeye maisha yake mazuri anaishi kwenye jumba kama yupo ulaya kumbe hako kajumba kenyewe hata ya baba yangu mdogo nzuri.
Kilikuwa kijumba kidogo cha vyumba vinne, vyumba vyenyewe vidogo sana na havikuwa hata na simenti.
Vidirisha vilikuwa vidogovidogo vya kizamani, nyumba haijapigwa hata plasta, vitofali vilikuwa vyeusi kutokana na moshi wa kibatari, yaani ilikuwa ni tafrani aiseee...!
Vyumba hivyohivyo vinne kapangisha viwili, kimoja ambacho ndio sebule alikuwa akilala mjukuu wake, Luis na kimoja ndio chake yeye yaani hicho ndo nikuwa natakiwa kuishi na mume wangu huyo.
Nisaidieni kushangaa wasomaji, hivi huyu mzee ana akili kweli! Kapata hela nyingi za mafao badala ya kujenga nyumba nzuri au hata kuikarabati hii na kuiweka katika hali nzuri badala yake anahangaika na wasichana kama mimi na kutumia mihela kibao, hivi ni akili au matope!
Kwa kweli maisha ya pale sikuyafurahia hata kidogo!
Hata hivyo sikuwa na jinsi kwani ndio yalikuwa makazi yangu mapya.
Hapo ndipo nikaanza maisha rasmi ya ndoa na kibabu kile.
Basi babu mwenyewe alikuwa kachoka yaani hakuwa na nguvu kabisa ya kunitekelezea mahitaji yangu katika suala nzima la malavidavi.
Je nini kiliendelea ? SHARE ILI TUZIDI KUPASUA ANGA!

0 Comments: