Monday, November 11, 2019

JIRANI, CHUMBA CHA PILI (13).

MTUNZI: AMMI CYPHER
AGE…(18+)
**********
Ni wiki sasa tangu Daniel ameanza kuishi kwa Careen siku hiyo wakiwa wameketi sebuleni wanaangalia TV series maarufu ya power Daniel akasema,
“Baby ila watu wanaofanya hizi biashara haramu wana maisha mafupi sana, angalia jinsi 50 cent alivyouawa na polisi hapo kikatili.
“Mmmh mmh!! Careen akajibu kwa kuguna,
“Yani kibaya zaidi unauawa inabaki picha mbaya kwa familia, kila wana ndugu wanapokatiza mitaani wananyooshewa…..”
“Danny!!!! Kwani huwezi kutizama movie bila kuzungumza” Careen akamkatisha hakutaka hadithi nyingi za Daniel kwani kitu alichokuwa akiambiwa kilikuwa na ukweli ndani yake.
“Sawa baby nisamehe, by the way kuna serious issue ningependa tuzungumze”
“Ishu gani hiyo?
“Baby unajua ni wiki sasa tangu nimefika hapa kwako, nimekuwa ni mtu wa kuamka, kula, kuangalia movie kama hivi na kulala hivi huko kwenye ofisi unayofanya kazi hakuna nafasi yoyote ambayo naweza kupata nikaondokana na kushinda nyumbani kutwa nzima”
“Huko ofisini kwetu kazi hakuna” Careen akamjibu Daniel kwa kumkausha
“Careen!” akaita Daniel
“Sema” huku macho bado yake yakiwa yanaangalia movie
“Nadhani hauko sawa, tutaongea basi vizuri baadae ukimaliza kuangalia hii series” Daniel akaondoka sebuleni hapo na kuelekea chumbani, Careen alikuwa amekasirishwa na kitendo cha Daniel kuweka mazungumzo marefu kwenye ishu ya kazi zake kwani kiukweli hapo mjini hana kazi yoyote anayoifanya ofisini zaidi ya kuwa transporter wa kusafirisha biashara haramu za madawa ya kulevya, Na biashara hiyo inahitaji umakini wa hali ya juu si ya kumueleza kila mtu hata wale unao waamini, ndio maana akaweka ukali kidogo Daniel alipokuwa anaomba kutafutiwa nafasi.
**********
Rose aliendelea na masomo yake chuoni hakutaka hata siku moja kufungua mdomo wake kwa rafiki zake kuwaeleza kwamba alikuwa mjamzito akazidi kukomaa na kitabu hakutaka kabisa ujauzito ule uharibu future yake aliyokuwa akiipambania kwa miaka mingi, akabaki kulificha ficha tumbo ili mtu yeyote asigundue. kila alipokuwa akimtafuta baba mwenye kiumbe chake cha tumboni amueleze hali ya afya yake hakuwa akipatikana simuni, hata alipoenda sehemu aliyokuwa akiishi aliambulia patupu, akabaki kukomaa na kusoma kwani zilibakia wiki tatu tu kuingia kwenye mitihani ya kumaliza chuo, japo muda mwingi pia alitumia kuwaza kuhusu Daniel apotee vipi katika mazingira ya kutatanisha kama yale ghafla tu simuni hapatikani, kazi pia aache bila taarifa rasmi, yalikuwa ni mambo ambayo alikuwa akiyawaza pindi alipokuwa akilitizama tumbo lake.
“Rose! Weee Rose! Amka umepatwa na nini”
“Jamani! Alikuwa anaenda pale stationary ku print assignment, sijui atakuwa ana tatizo gani embu mshike miguu tumuinue tumpeleke hospital” Yalikuwa ni maongezi wa wanafunzi wenzie Rose baada ya kuanguka ghafla alipotoka kundini hapo akiwa anaelekea stationary,
Wakamchukua wakampakiza kwenye gari la mwanakundi mwenzao, haraka kuelekea hospitali
“Nani rafiki yake wa karibu kati yenu? Aliuliza dokta baada ya kutoka kwenye chumba alichopumzishwa Rose,
“Ni mimi hapa” akajibu mwanadada Jackline ambaye ndiye wanalala chumba kimoja hostel
“Naomba njoo ofisini tuzungumze kidogo” akasema dokta huku akielekea ilipo ofisi yake,
“Umesema wewe ndiye rafiki yake wa karibu?
“Ndiyo”
“Sawa, hali yake si mbaya sana, ila alikuwa tu amepungukiwa maji na ndicho kilichopelekea akapoteza fahamu, na Je ulikuwa ukifahamu kama rafiki yako ni mjamzito”
“Mmh! Mh! Hapana, hakuwahi kuniambia na licha ya hiyo sidhani kama yeye pia alikuwa akifahamu kuhusu hali yake, kwa maana ni mtu wa karibu sana kwangu na si mtu wa kukaa na kitu moyoni kiasi hicho”
“Ok, maadamu wewe ndiye rafiki yake wa karibu natumaini utamuweka sawa, embu jaribu kumfanya awe anakula chakula vizuri na kwa wakati, pia jaribu kukaa nae karibu asiwe mtu wa stress, kwa sasa tutampumzisha kidogo ila baadae nadhani mtarudi nae chuoni.
Jioni Rose akaruhusiwa kutoka, baada ya kufika chuo rafiki zake wakamsaidia mpaka akafika chumbani kwake anakoishi yeye na Jackline,
“Jamani ngoja sisi tukamalizie ile kazi muda huu maana lecture Shitete kwa kutoa ziro hajambo, japo sidhani kama tutamaliza mapema mana mtu ambaye huwa tunakutegemea kwenye ku type ndo hivyo tena hauko vizuri”
“Hahahah ha!!! Sawa Farid ila leo ndo mtatambua kuwa kuna umuhimu wa kila mwanakundi kuongeza juhudi katika mazoezi ya ku type, siyo kila siku tumtegemee Rose na haya ndiyo matokeo yake” akajibu Jackline
Baada ya wanafunzi wengine kuondoka, wakiwa wamebaki wawili tu chumbani kwao, Jackline akasema
“Pole sana Rafiki yangu kwa sasa unajisikiaje?
“Aaah Jack bhana, mi siumwi sana kiasi hicho, najisikia kuchoka tu maana kubeba hiki kitu siyo mchezo”
“Yani best ndo ukanificha hata mimi looh! Kweli saizi hatuaminiani kabisaaaa yani tunalala pamoja kuamka pamoja, darasani pamoja, group discussion pamoja yani kama mapacha, kila sehemu pamoja lakini bado ukanificha, lakini siyo mbaya ndo ishatokea”
“Nisamehe rafiki yangu ila sikutaka tu nikubebeshe majukumu mapya ya kuniangalia kwa ukaribu hasa ukizingatia tena kipindi hiki cha kuelekea mitihani ya mwisho”
“Hata kama Rose, lakini bado mimi ndiye rafiki yako wa pekee, kama ungepatwa na jambo kubwa zaidi ya hili mimi ndiye ningekuwa wa kwanza kuulizwa, hayaaaaa twende mbele turudi nyuma shosti, nani ni muhusika wa hili jambo?

Previous Post
Next Post

0 Comments: