Monday, November 11, 2019

CHOMBEZO :MAMA MWENYE NYUMBA

Image may contain: one or more people, people sitting and text
EPISODE :01
“Mke wangu, kila siku namwona huyu kijana mchafuchafu anakuja kuokota chupa tupu hapa, ina maana tuna chupa tupu kila siku?”
“Siyo hivyo mume wangu, we hujamfuatilia tu, anakuja kila baada ya siku tano. Tumsaidie mume wangu, si unamwona kijana mwenyewe maskini huyu,” alisema mama Joy huku macho yake yote yakimwangalia yule kijana mwokota makopo…
“Awe anakuja mchana basi, usiku kama huu hapa nje, mimi naweza kumchapa risasi nikidhani mwizi. Si unaona hata mavazi yake? Kwanza haogi huyu, hata harufu anatoa
“Mume wangu usimkufuru Mungu, sisi kupewa uwezo ni matakwa yake, hakuna binadamu ambaye akipewa nafasi ya kuchagua maisha bora na duni, atasema anataka duni.”
“Mimi sijafika huko, ila nasema awe anakuja mchana tu si usiku kama huu.”
“Sawa mume wangu,” alisema mama.
Hayo yalitendeka wakati baba Joy akiegesha gari mahali pake kisha akashuka na kuanza kutembea mkononi ameshika brifkesi yake.
Siku hiyo, baba Joy alikuwa kama amevaa Kinaijeria f’lani.
Mama Joy alimpokesa mumewe brifkesi kisha akamwacha apite ili yeye amfuate kwa nyuma. Wakati mumewe anaingia, mama Joy aligeuka kumwangalia mwokota chupa tupu ambaye kwa muda huo alikuwa amebeba fuko la ‘salfeti’ begani.
Mama Joy alimwonesha ishara kwamba aondoke haraka sana kwa vile mumewe amerudi. Kijana wa watu, alitoka getini kwa kuruhusiwa na mlinzi.
“Unasikia mama Joy,” baba Joy alianza kusema tena akiwa amekaa kwenye sofa kubwa…
“Abee…”
“Mimi sipendi watu wawe wanaingiaingia humu ndani hovyo. Tena nadhani iko haja ya sehemu ya kutupia taka niijenge nje ili watu wasipate sababu ya kuingia ndani…
“Wewe kijana mchafuchafu vile, si lazima pia atakuwa mwizi..?”
“Nimekuelewa baba Joy, hataingia tena usiku ikitokea akaingia humu basi itakuwa mchana.”
“Iwe hivyo, sitaki kumwona tena usiku. Kwanza wewe ni mke wa mtu, mnachekeanachekea kwa sababu gani?”
“Basi mume wangu jamani, nimekuelewa.”
Mzee huyo aliondoka kwenda kazini, mkewe mama Joy alisimama nje kwa muda mrefu, alipotaka kugeuka kurudi ndani, kwa mbali alimwona mwanaume akitokea. Mgongoni alibeba furushi…
“Au yule?” alisema moyoni. Alisubiri kwa muda ili amwone kwa karibu, lakini hakuwa yeye.
Nusu saa baada ya kuingia ndani, kengele ya geti kubwa ililia…
“Mh! Si yeye huyo?” alijihoji mama Joy akiamini aliyebonyeza kengele ni mzoa taka. Japokuwa alijua mlinzi atashughulikia, lakini aliamua kutoka mwenyewe kuelekea getini ambapo alimkuta mlinzi anasukuma geti kubwa.
“Nani amepiga kengele?” mama Joy aliuliza…
“Sijamjua ni nani?” mlinzi alijibu huku akiendelea kusukuma geti, likawa wazi…
“Shikamoo mama,” mzoa taka alisalimia akiwa anatabasamu...
“Hujambo wewe?” mama Joy alijibu hivyo badala ya kusema marhaba. Na tangu mzoa taka huyo ameanza kuingia ndani ya nyumba hiyo kuchukua taka, kila akimsalimia shikamoo mama Joy anajibiwa hujambo wewe au asante kijana…
“Sijamboo, shikamoo…”
“Asante…askari, funga geti…”
“Sawa. Huyu mzoa taka aingie..?”
“Aingie ndiyo. Akishaingia funga geti.”
Mzoa taka aliingia hadi ndani, akamkaribia mama Joy ambaye naye alimkaribisha hadi kwenye sehemu yenye taka.
Mlinzi aliwakodolea macho. Kilichomshangaza zaidi ni kauli ya baba Joy kwamba hataki kumwona mzoa taka huyo nyumbani kwake…
“Sasa mbona amemuingiza tena leo? Halafu kuna siri nzito mimi naiona kati ya mama na huyu mzoa taka, maana mama akiamkiwa shikamoo hatakagi kuitika marhaba,” mlinzi aliwaza.
Mama Joy alimfikisha mzoa taka kwenye pipa la taka ambalo lilijengwa vizuri ndani ya nyumba hiyo…
“Jana mwenzangu mzee alikasirika sana,” alianza kusema mama Joy…
“Hata mimi kama nilimwona. Niliogopa sana…”
“Yeye anasema hataki kuona unaingia humu ndani usiku. Akasema atalitoa hili pipa na kulijengea nje huko.”
“Kwa hiyo akinikuta saa hizi humu ndani kwake si ataniua?”
“Hawezi, ingawa ana bastola…”
“Mama mimi nakwenda, kumbe mumeo ana bastola..!”
“Hawezi kukuua, alisema hataki uingie usiku, ‘asa kwani saa hizi ni usiku?” alisema mama Joy huku akimsogelea mzoa taka huyo na kumshikashika kidevuni. Alizikuna ndevu zake chache…
“Una ooo nzuri kijana, sema tu hutaki kuitunza…”
“Una macho mazuri, madogoooo, sema tu unayashindisha juani mpaka yanakuwa mekundu, au unavuta bangi..?”
“Sivuti bangi mama…”
Je nini kiliendelea SHARE KWA WINGI ILI UIPATE KWA WAKATI
Previous Post
Next Post

0 Comments: