Monday, October 28, 2019

SIMULIZI KWA WANANDOAA

Image may contain: 1 person, standing
Mwanaume mmoja alirudi kutoka kazini akamkuta mke wake yuko jikoni anapika
Mume alimkumbatia na kumpa busu moto moto.

Wakiwa kwenye meza tayari kwa chakula cha jioni simu ya mwanamke ililia ukaingia ujumbe kutoka kwa rafiki yake akimtakia usiku mwema
Mume alipouona akaudhika na kususia chakula akainuka kimya kimya akaenda kulala.

Mke naye hakufurahishwa na kitendo alichokifanya akajisemea moyoni, yaani mtu mzima unazira na ujumbe mdogo kama huu mimi siwezi kukufata wewe sio mtoto mdogo hata kidogo.

Mwanamke alikula peke yake na alipomaliza alienda kulala, walilala kwa kugeuziana migongo.

Usiku wa manane mwanamke alishikwa na homa kali mwili ulitoka jingi mno. Alishindwa hata kuongea, alipojaribu kumtikisa mume wake mume bado alikuwa amezira alimsukuma mwanamke mikono yake bila hata kuongea neno lolote. Mke aliendelea kuhangaika mwisho akashindwa kupumua na kufariki kwa kiharusi.

Asubuhi mume aliamka na kuanza kujiandaa kwenda kazini alimwangalia mke wake akamwona bado amelala ila alimuona kama amejinyosha sana lakini akapotezea akajisemea: staki kuongea naye mpaka atakaponianza.
Alivaa nguo akaenda kazini.

Wakati wa mchana alipokua anarudi nyumbani aliamua kununua saa nzuri ya kama zawadi ya kurudisha amani kwa mke wake.

Aliwasili nyumbani akiwa na furaha akiamini mke wake atafurahi pia kwa zawadi aliyomletea na alikuwa amejipanga kwenda kumhakikishia mke wake wake kuwa anampenda kwa dhati.

Alipofika nyumbani alifungua mlango moja kwa moja akaelekea jikoni alijua kuwa mke wake atakuwa anapika kama kawada yake ajabu hakumkuta, akaenda chumba akamkuta mke bado amelala kwa staili ile ile aliyomuacha asubuhi

Mume alishtuka sana na alipomfunua shuka akagundua mke wake amekufa tangu asubuhi.

Hili ni fundisho hasa kwa wapenzi mnachukizana kwa vitu vidogo vidogo na kusahau upendo na mema mnayofanyiana siku nyingi.

Pongezi nyingi kwa wote mnasapoti page hii, like na coment zenu zinatia moyo kuona kweli kazi yangu inapokelewa. Asanteni sana Mungu awabaliki.
Previous Post
Next Post

0 Comments: