Mama mmoja alienda kanisani akawaacha watoto wake nyumbani.
Watoto wake walikuwa watatu, wakwanza alikuwa na miaka 6, wapili miaka 4, wamwisho miaka 2 na miezi 8
Mama huyo aliwabusu wanae ishara ya upendo na kuwaacha akaenda kanisani.
Yule mtoto wa mwisho alishika pasi na kuigusisha kwenye nyaya za umeme akapigwa shoti, kaka yake alipomuona amenasa kwenye umeme akajaribu kumuondoa nae alirushwa mbali na kupoteza fahamu, mtoto aliyebaki akaanza kulia kwa nguvu majirani walipokuja wakaita ambulence yule mtoto akapelekwa hospitali.
Mama aliporudi kutoka kanisani alielezwa kilichowakumba watoto wake akakimbia kuelekea hospitali, alipofika hospitari alikuta tayari mtoto wake ameshafunikwa shuka nyeupe ikimaanisha ameshapoteza uhai.
Mama huyo alipiga magoti na kusali:
Bwana Yesu sikuwa nimeenda kufanya ukahaba, nilienda kulitumikia jina lako na nikawaacha watoto wangu chini ya uangalizi wako, kwanini unaniadhibu, kama kuna jambo nimekukosea Bwana wangu naomba unisamehe, msamehe pia mwanangu.
Wakati anaendelea na maombi mtoto alipiga chafya na kukohoa, docta hakuamini akajikuta akisema: haiwezekani mtoto nimempima nikahakikisha amefariki halafu apone!! Mama akiwa analia akamjibu: hakuna lisilowezekana kwa Mungu
Mungu awabariki wote mtakaosoma ujumbe huu na asanteni sana wote mnaosapoti page hii, tupo pamoja daima.
Kama unamwamini Mungu andika #ameni na unaweza ku share katika magrup mengi
By Joseph Lawrence Jigalu
0 Comments: