Nilinyanyuka Kitandani nikiwa sijitambui vizuri, nilikua nikiwaangalia watu kama wagani wageni hivi. Mama yangu alikua kaaa pembeni yangu. “Wewe si utoke nnje, kwanini unalia mbele ta mtoto?” Baba yangu alifoka. “Wewe ndiyo umemfanya hivi mtoto mpaka hamsikilizi mume wake, wanawake ni wajinga sana, unaona sasa umemsababishia Baba wa watu matatizo mpaka sasa yuko jela!” Baba alifoka, bado nilikua sijajua ni kitu gani kilikua kimetokea, bado nilikua na mshituko mkubwa.
“Akafie mbeli, unaona kitu alichomfanya mwanetu, hivi wewe Baba Amina (Sio jina Lake Halisi) inamaana huna uchungu kabisa na mwanao?” Mama aliongea kwa uchungu sana, nilimuona Baba akimsogelea, alichukua mkono wake wakulia, akaupeleka shingoni kwa Mama, hapa kwa nyuma chini kidogo ya kisogo. Ni kama mtu alikua anamshikashika tu lakini alimbonyeza kwa nguvu mpaka Mama akaanza kupiga kelele. “Nakufaaaa!” Mama alipiga ukulele huku akinyanyuka kutoka kitandani, wagonjwa wengine walishtuka na kugeuka kuangalia.
“Unanikosea adabu, nimeshakuambia kuwa usiwe unanijibu jibu, au unafikiri kuwa siwezi kukupiga kwakua tuko mbele za watu. Nitakuua na kama ni kufungwa nikafungwe mshenzi mkubwa wewe!” Baba alifoka huku akimuachia Mama, alitoka pale hospitalini na sikumuona mpaka niliporuhusiwa kutoka hospitalini wiki mbili baadaye. Nilirudi nyumbani nikiongozana na Mama, nilipofika tu, ile kutaka kuingia Baba alikua mlangoni.
“Unaenda wapi?” Aliniuliza, nilinyamaza kimya nikimuangalia Mama anisaidie kujibu, lakini hata yeye alionekana kuogopa, akanyamaza kimya. “Wewe si ulishatolewa mahari? Unataka nini hapa? Mume wako alikuja kukuchukua kwangu, kama hajakuchoka, kama hajakurudisha basi siwezi kukupokea!” Aliendelea kufoka, Mama aliniangalia, macho yake ni kama yalikua yananimbia “Ondoka mwanangu, sina chakukusidia.” Bado nilikua sijapona vizuri, nilriruhusiwa kutoka hospitalini kwakua nilipata nafuu kidogo na Mama hakua na pesa nyingine ya kulipia kuendelea kulazwa hospitalini. Mume wangu ndiyo kabisa alikua hataki kabisa kunisikia.
Bado alikua ananilaumu kwa kumsababishia kuwekwa mahabusu kwa wiki mbili baada ya kunipiga. Ingawa si mimi nilienda kumshitaki lakini alikua akilalamika kuwa kama nisingepiga kelele wakati ananipiga basi asingekamatwa na kuwekwa ndani. Haikua mara yake ya kwanza kunipiga, mara zote wakati akinipiga nilikua nanyamaza kimya, alikua akikasirika sana kama nikipiga kelele akisema kuwa ninachonganisha na watoto hivyo hataki kabisa nipige kelele.
Lakini siku hiyo ilikua tofauti, nakumbuka nilikua sebuleni, mume wangu alikua anaangalia mpira. Wakati anaangalia umeme ulikatika, alianza kuwalaumu TANESCO kwani mume wangu anapenda sana mpira. Lakini mtoto wangu mdogo aliropoka.
“Luku itakua imesha, mbona kwakina Kelvin (sio jina halisi) unawake…” Mume wangu alinyanyuka taratibu, aliwasha simu yake ya tochi na kuniita chumbani, nilienda nikikimbia, mpaka wakati naingia sikujua kama ninakosa na wala sikujua kama naenda kupigwa kwani mume wangu siku hiyo alikua katika mood nzuri.
Lakini ile naingia mlangoni nilisikia “Paaa!” umeshawahi kufungua mlango nusu, halafu ukaufunga kwa nguvu, basi ndiyo kilichotokea, mume wangu alikua kasimama nyuma ya mlango, aliufungua nusu na nilipoingia aliubamiza kama vile anaufunga, haukufungika bali mlango ulinipiga usoni, pua mdomo vilianza kutoa damu.
“Nakufaaa!” Nilipiga kelele.
“Unakufa! Hivi wewe ni mwanamke wa namna gani? Una kazi gani nyingine unanya hapa nyumbani! Yaani mimi narudi nyumbani, nataka nikae na familia yangu, lakini nawasha TV, umeme umekatika, najua ni TANESCO nalaumu serikali kumbe ni wewe mshenzi umeshindwa kuniambia kuwa umeme umeisha nikanunua umeme!” Alifoka kwa nguvu, mpaka wakati huo ndiyo nilikua nimetambua kosa langu, sikua na kitu kingine zaidi ya kuomba msamaha.
Nililazimika kunyamaza kimya bila kuseama chochote, maumivu niliyokua nayo yalikua hayaelezeki, lakini nilijua kuwa, kama nikiongea, kama nikilia, kama nikipiga kelele basi mume wangu angeniua. Mume wangu ni mtu wa hasira sana na nilijua kabisa kuwa hawezi kuniacha kama nikipiga kelele.
“Nisamehe mume wangu nilipitiwa…” NIlijitahidi kuongea huku nikizuia sauti yangu isilete mikwaruzo ya maumivu.
“Ulipitiwa? Ulikua unafanya nini tangu asubuhi ukashindwa hata kuangalia kuwa umeme umeisha?” Aliniuliza, nilikua na mengi ambayo nilikua nayafanya na ningeweza kumjibu lakini nilijua fika kuwa mume wangu hahitaji hayo majibu, alichokua anataka yeye ni mimi kumuambia umeme umeisha, anunue basi, hayo mengine hayamhudu.
“Hapana mume wangu, nisamehe, sitarudia tena…” NIlijitetea, alinyanyua kitocho chake cha simu na kunipiga usoni.
“Kwahiyo umepasuka pua ili nionekane nakupiga? Unataka watu kuniona mimi mbaya eeeh! Unataka utoke hivyo watoto waone nakupiga wanichukie mimi Baba yao?” Alifoka.
“Hapana mume wangu, nisamehe…”
“Kila siku wewe ni kuomba msamaha, hivi kwanini huna akili, hivi kwanini nimeoa mwanamke mpumbavu namna hii? Hivi unafikiri ningeoa mwanamke ana akili si ningekua mbali, wafanyakazi wenzangu waliooa wanawake wa maana sasa hivi wana maisha mazuri lakini wewe ni sifuri kabisa!”
Aliendelea kufoka, nilinyamaza kimya nikimsikiliza, kwakawaida akiongea huwa hataki kukatishwa.
“Unaombaomba misamaha kila siku, mimi naona bora tuachane, nikurudishe kwenu ukaendelee na umasikini wenu, maana nimechoka, kubeba mwanamke ambaye hana akili ni upumbavu!” Aliendelea kuongea, pamoja na kwamba hasira zilinipanda, pamoja na kuwa katika maumivu makali lakini sikuweza kuongea chochote.
“Nimekusamehe kwakua ni kosa langu mimi kuoa mpumbavu, wakati wenzangu wanaoa wake mimi nikaoa taahira.” Nilishukuru Mungu, niliendelea kubaki pale nikisubiri maelekezo mengine,
“Unaweza kununua umeme kwenye M-Pesa?” Aliniuliza.
“Ndiiyo naweza, nilijibu harakaharaka, alinipa simu yake na kuniambia ninunue umeme, niliichukua na kununua umeme. Yeye alitoka na kurudi sebuleni, kama dakika kumi baadaye alirudi.
“Ushanunua?” Aliniuliza.
“Ndiyo lakini bado hawajanirudishia meseji.” NIlimjibu huku nikimkabidhi simu yake, aliichukua na kuangalia salio.
“Wamekata lakini…”
“Ndiyo labda itakua ni network.” Nilimjibu, alirudi sebuleni, alikaa tena kwa kama dakika ishirini na kurudi tena kuniulizia.
“Simu si uko nayo wewe mume wangu, mimi sijui kama wamesha tu….” Sikuweza kumalizia, nilikua nimekaa kitandani nilishangaa mtu amenikanyaga tumboni. Kabla hata sijajipanga kuwaza naumia vipi nilisikia ngumi ya sikiko la kushoto. Nilikua nimekaa lakini nilipatwa na kizunguzungu, kilichofuata hapo ni kipigo cha Mbwa Koko! Wakati wote huo mume wangu alikua akinipiga huku akilalamika kuwa nimenunua umeme vibaya mimi halafu nampiga hovyo. Sikujua ni wakati gani nilipiga kelele, sikujua nini kilitokea, lakini nilikuja kuzindika wiki moja baadaye nikiwa hospitalini.
Mume wangu alikua kakamatwa na Polisi, sijui ni nani aliita watu lakini Polisi walijua kuwa nitakufa ndiyo maana hawakutaka kumuachia, pamoja na kuhonga, pamoja na mume wangu kujuana sana na Polisi kwani yeye ni mwanajeshi na ana cheo kikubwa tu lakini waligoma kumuachia wakijua kuwa ni kesi ya mauaji. Baada ya mimi kuzinduka ndipo walimtoa kwani ilikua si kesi ya mauaji tena bali ikabadilika na kuwa kesi ya kumpiga mke. Pamoja na Baba kujua yote hayo lakini bado alitaka nirudi kwa mume wangu.
“Baba Amina, mruhusu basi mtoto angalau alale kwa leo, hali yake bado haijatengamaa…” Mama alijitahidi kuongea, nilimuona jinsi alivyokua anaumia, namna alivyokua akilengwalengwa na machozi. Nilijihisi vibaya kwani nilijua lazima Baba atakataa na angeweza kumpiga Mama kwa hilo.
“Hapana, Mama, niko sawa, hali yangu ni nzuri, niache nirudi kwa mume wangu, nimewamiss wanangu.” Niliongea kwa shida sana, bado mwili wangu ulikua katika maumivu makali, hata kupumua ilikua shida sana achilia mbali kuongea.
“Unaona, mtoto mwenyewe anasema kapona lakini wewe kiherehere chako ndiyo unaingilia ndoa za watu wakati yakwako imekushinda, muache arudi kwake, kama mume wake kamchoka atamrudisha!” Baba aliongea, safari ya kurudi nyumbani ilianza. Mama alitaka kunisindikiza lakini Baba alikataa, alimuambia ana njaa.
“Yaani wiki ngapi hizi uko hospitalini unamuuguza mwanao, namimi nataka kuhudumiwa au unafikiri nilikuoa ili nije kujipikia mwenyewe. Huyo anapajua kwake, muache aende, hatakiwi kupelekwa.” Mama aliingia ndani, mimi nilijikusanya kusanya na kuondoka kurudi nyumbani kwangu.
Ilikua ni siku ya kazi hivyo nilijua kuwa wanangu watakua shuleni na mume wangu naye atakua kazini. Nilifika na kukuta milango iko wazi, nilijua kuwa nitakunana na binti wa kazi, niliingia getini, nikaenda mpaka ndani, niligonga kwa uoga nikijua kuwa kama kwa bahati mbaya mume wangu akiwa njiani nikiingia bila kugonga ningekutana na kipigo.
“Unataka nini wewe Mwanamke, hivi kwanini hukubali kuwa hupendwi, mwanaume anakupiga kutaka kukuua lakini bado upo tu?” Mlango ulifungulia, hakuja binti wa kazi au mume wangu bali alikua ni Sakina (sio jina lake halisi).
Ni mchepuka wa mume wangu wa muda mrefu, mara nyingi nilikua nikimfumania na mume wangu naishia kupigwa, nilishakuta mesji nyingi akimtumia mume wangu, picha zake nyingi za uchi na nikiuliza naishia kupigwa. Nilishangaa anafanya nini pale, tena akiwa kava shati la mume wangu na chini hamna kitu, yaani ni kama alikua uchi tu. Alionekana kama anaishi pale, nilishangaa kwakua Sakina alikua ni mke wa mtu, tena mke wa mmoja wa marafiki wa mume wangu, nilishangaa nikiwaza kama ndiyo kaachika na mume wangu kamuoa au?
Amina anarudi kwake baada ya kipigo cha nguvu kutoka kwa mume wake, bado hajapona vizuri anakutana na mwanamke mwingine nyumbani kweke. Mimi sisemi, ila muambie kuwa kuna simulizi nyingine ambayo ndiyo kwanza imeanza. Hivyo mtag na muambie aendelee kufuatilia ukursa huu
0 Comments: