Monday, October 28, 2019

PINGAMIZI LA NDOA KANISANI

Image may contain: 2 people, people standing
"Kama kuna mtu anapinga kuwa hawa wawili hawafai kufunga ndoa ajitokezee"

Nisauti ya mchungaji aliekua akiwaambia watu waliofika kanisani hapo ili kushuhudia ndoa ya wawili hao wapendanao.Kanisa lote kimyaaa,.Mchungaji akarudia tena.

"Kama kuna mtu mwenye pingamizi kuwa wawili hawa hawapaswi kufunga ndoa anakaribishwa.

Kanisa lote kimyaaa,mchungaji akarudia tena na tena.Kanisa lote kimyaa,kimyaa,kimyaaa.

Ghafula ukimya ule wa waumini,ukaingiliwa Kati na binti albino aliekuwa amebeba mtoto wake mgongoni,akaanza kuzipiga hatua kutoka benchi la mwisho kuelekea mbele.Watu macho Kodo,wengine waliinamisha vichwa vyao huku wengi wao wakisubiri kwa hamu kusikia ni pingamizi gani hilo.

Bwana harusi alipo muona binti yule albino akija akaanguka puuu! akazimia,kanisa lote likanyanyuka likaitikia "wooooooooooooo😱😱😱" msaidizi wa bwana harusi akakurupuka ghafula kukimbia alivyo na bahati yake mbaya watu wakamudaka.Msaidizi huyo wa bwana harusi akapaniki,akaanza kupiga makelele akisema.

"Siyo mimi niliyekubaka,ni Charles aliagizwa na Mganga ili apate mali"

Bibi harusi kusikia hivyo akaanguka "puuu!" akazimia kwa sababu Charles ndo alikua Bwana harusi,kijana mtana shati na tajili kanisani,Kila kona kukawa ni vilio vya wazazi na ndugu wa maharusi.

Baadae kukawa na utulivu uliopatikana kwa jitihada kubwa,mchungaji akaendeleza majukumu yake,Akamuuliza yule binti albino.

Ni kweli kuwa ulibakwa?

Binti akajibu "Ndiyo nilibakwa miaka miwili iliyo pita na ndo matokeo ya huyu mtoto, sikufanikiwa kumjua mbakaji,lakini nilimuomba Mungu siku moja amfunue baba wa mwanangu.
Mchungaji akauliza tena "kama hukumjua mbakaji kwanini ulinyanyuka kuja kutoa pinga mizi?"

Binti akajibu

Nilikuwa siji kutoa pingamizi,nilikuwa nakuja kukaa huku mbele huko nyuma sisikii wala kuona vizuri.
😝😝🤣🤣😆😆😂😂🤣🤣😝
Previous Post
Next Post

0 Comments: