Monday, October 28, 2019

FUNZO KUBWA SANA HILI

Mwanamke mmoja alikuwa akifanya kazi katika
kiwanda cha kusindika nyama. Siku moja baada
ya kumaliza kazi zake pale kiwandani alienda
katika chumba chenye freezer (cold room)
ambako nyama zilikuwa zikihifadhiwa kukagua
vitu fulani. kwa bahati mbaya wakati yupo
kwenye hicho chumba cha ubaridi mlango
ulijifunga na kijilock kwa nje. na hakukuwa na
msaada wa kuweza kuufungua mpaka kuwepo
mtu wa nje.
Ingawa alilia na kupiga kelele za kuomba msaada
wa kufungiliwa lakini kelele hizo hazikuwa rahisi
kusikika nje ya hicho chumba kidogo, na
wafanyakazi wengi pale kiwandani walikuwa
washaondoka.
Masaa matano baadae akiwa katika hali ya
kukaribia kukata roho kutokana na baridi kali ya
hicho chumba, mlinzi wa geti la kiwanda hicho
alifungua mlango wa cold room alimokuwamo
yule mwanamke. Na baadae baada ya kutolewa
na kupata nafuu alipata wasaa wa kumuuliza
yule mlinzi ilikuwaje na akafungua mlango wa
cold room wakati ilikuwa si ratiba yake na vile
vile si kazi yake?.
Maelezo ya yule mlinzi, ''nimefanya kazi kwenye
hichi kiwanda kwa miaka 38 sasa, mamia ya
wafanyakazi wanatoka na kuingia kiwandani
lakini wewe peke yako kati ya wote uliyekuwa
ukithubutu kunisalimia asubuhi na kuniaga kila
jioni unapoondoka kiwandani, wengine wanani-
treat kama mtu nisye na thamani na ambaye sipo
katika ulimwengu huu.
Leo ulipokuja kazini asubuhi ulinisalimia kama
kawaida ya tabia yako ya kujali ilivyo ''uliniambia
habari za asubuhi na tukafurahi kwa dakika mbili,
lakini leo baada ya muda wa kazi kuisha sijapata
kwa heri yako na ile ya kunitakia joni njema na
kubaki salama. Hivyo nilachukua uamuzi wa
kuzunguka kwanza humu ndani kuangalia kama
upo kwa sababu kujali kwako kumekuwa
kukinifanya na mimi nionekane ni mtu katika
ulimwengu huu.
Kwa kutokupata farewell yako siku ya leo
nikagundua tu kuna baya litakuwa limekupata. na
ndipo nilipokukuta kwenye chumba cha barafu.
FUNZO
Ishi vizuru na kila mtu, be humble to every one,
mheshimu kila mtu wakubwa na wadogo. Try to
have an impact on people who cross your path
every day kwa sababu huwezi jua kesho yako
imebeba kitu gani.
Share share share share
Na wengine wajifunze
Previous Post
Next Post

0 Comments: