Monday, October 28, 2019

©Nitazame Mwanangu ©

Nakuomba unitazame mwanangu ni Mimi huyu huyu niliebeba mimba miezi tisa, nilivumilia sana mpaka siku nilipojifungua. Nilitamani unione enzi za ujana nilivyokuwa Mrembo, tazama Leo nimebakia mifupa Natia mpaka huruma, kifo ni haki yangu, jamii imetupiga teke viongozi wakatumwagia maji yaliojawa na ukoko.

Mwanangu tazama ninavyotisha Mama yako, Mpaka watu wamediriki kuniita msukule naumia sana, zamani niliweze kujishugulisha nakuokota chochote kitu hukuwahi kushinda pasipo chakula.

Nasikitika sana mwanangu tajiri yule aliyenipa ujira katika kiwanda chake Leo kawa adui Mkubwa kwa kiranja anaeongoza eneo letu la usafi, kiranja amekosa busara ata ukiwahi Namba anasingizia hujabeba ufagio zote hizo ni ila za kikwapa kunuka pasipo kidonda.

Mwanangu siwezi kupona tena Nina kufa nikiwa na hasira sana na yule Bwana ila mwambie ipo siku tutaonana atanieleza ni kwanini anajificha kwenye kichaka cha kupenda wanyonge, ni wanyonge gani Labda aniambie. Mateso nayoyapata mwambie namsubiri arudi uraiani tucheze ile ngoma ya kwetu. Ngoma ya ajabu iliyojawa na huzuni ya milele, mwanangu kwa kheri, Dunia kwa kheri acheni nipumzike.

#fasihi Tamu#
Previous Post
Next Post

0 Comments: