Monday, November 11, 2019

JIRANI, CHUMBA CHA PILI (07).


MTUNZI: AMMI CYPHER
AGE…(18+)
Ilipoishia…
“Naomba umsikilize mwenzangu hapo, kisha atakachoagiza utatuleta chumba cha Sokoine pale”
Sarah Mwakalinga akamwambia mhudumu, Daniel akaonekana kushtuka baada ya kusikia habari ya chumba.
“Naomba short ya taquira”
ENDELEA NAYO:
Ni siku ya pili sasa, bwana Sese anamuona mke wake ni mtu wa ndimu pamoja na maembe mabichi, na baadhi ya mambo mengine pia anayaona, ni mtu mzima anajua dalili za mwanamke mjamzito ila hakutaka kumuonesha mkewe kwamba ameshtuka, akatulia kama bado hajajua kitu,
“baby leo nimeamka ninajisikia vibaya mno, kichwa kinaniuma sana” bwana Sese akaanzisha maongezi
“Pole mume wangu, yani unavyochemka hii itakuwa malaria itabidi uende hospitali” akajibu Aisha huku akimgusa gusa mumewe mashavu na sehemu za shingoni.
“Siyo niende sema itabidi twende, we si mke wangu wewe ndo unatakiwa kujali zaidi afya yangu Aisha”
“Sawa mume wangu, jiandae basi twende sasahivi si unajua sipendi kukukera” Aisha naye akajibu huku akiinuka kitandani.
Basi baada ya wanandoa hao kujiandaa wakatoka nje wakasimamisha bajaji wakapanda, safari ya hospitali ikaanza, wakiwa kwenye bajaji bado Aisha aliendelea kutafuna embe lake, bwana Sese alibaki kumtizama tu bila kusema chochote akasubiri wafike hospitali wakajue yote huko.
Baada ya kufika eneo la hospitali wakashuka kwenye bajaji wakalipa wakaingia ndani wakakuta foleni kwenye mlango wa dokta, basi na wao wakaketi kusubiri zamu yao ifike, kwakuwa bwana Sese alikuwa anafahamiana na dokta Lucas katika hospital hiyo alimpigia simu asubuhi ya siku hiyo akamueleza kinagaubaga kuhusu swala lake na mkewe kwahiyo mpaka muda huo Aisha hakuwa akijua target ya kuwa hospitalini hapo ni kuhusu yeye kupimwa afya, Baada ya dakika kadhaa zamu yao ikafika wakaingia wote kwa pamoja kwenye chumba cha dokta,
“Ohooo! Ndugu yangu Martin Sesemkwa karibu, Shemeji karibu”, kwa uchangamfu dokta Lucas huku akiwapa mikono akawakaribisha, baada ya kuketi bwana Sese akasema,
“Dokta kuna wagonjwa wengine hapo nje wanataka huduma pia, kwahiyo ni vema tukafanya tu lile tulilokusudia kisha we ukaendelea na majukumu mengine”
“Aisha mke wangu mi si mkatili kiasi hicho nikuone una hali tofauti na ilivyo kawaida alafu nikafumbia macho swala hilo nitakuwa siyo mkamilifu, nimekuleta hapa nia na kusudio nije nifahamu afya yako, na siyo kwamba nimekuja kujua afya yangu mimi” bwana Sese akiwa kamgeukia mke wake aliongezea, maneno yaliyomfanya mke wake kushtuka sana mana ni kitu ambacho hakukitegemea hata kidogo kama kingetokea akaanza kutetemeka, lakini hakuwa na namna kwakuwa alikuwa ameshaingia kwenye mtego akakubaliana na mumewe, basi dokta Lucas akafanya kazi yake, kisha akawaomba wampishe kidogo aendelee, baada ya dakika kadhaa dokta Lucas akawaita waingie,
“Ni kweli bwana Sese kama ulivyodhani ndiyo hali halisi mkeo ni mjamzito, tena wiki mbili”
Bwana sese hakutaka maelezo zaidi akamshukuru dokta Lucas kisha akamshika mke wake mkono na kuondoka hospitalini hapo.
Baada ya kufika nyumbani bwana Sese akamtupa Aisha kitandani akavua mkanda wa suruali akamwambia,
“Aisha usiponiambia ukweli leo nitakuua, sema vizuri nani mwenye huu ujauzito”
“Mume wangu huu ni ujauzito wako, sasa wewe ndiyo mume wangu na tunaishi pamoja swali gani hilo unaniuliza” akajibu Aisha huku akipandisha sauti juu,
“Kama ni ujauzito wangu sasa kwanini hujaniambia, na ulikuwa unajua fika wewe ni mjamzito”
“Mume wangu niilitaka tu nikufanyie surprise” alisema Aisha huku akiwa kamsogelea mume wake na kuanza kumkumbatia, ghafla bwana Sese akabadilika akamsukuma mkewe kitandani akauzungusha mkanda vizuri kwenye kiganja cha mkono akaanza kumpiga nao, alimpiga mno lakini bado Aisha akashikilia msimamo wake kuwa ile mimba ni ya mumewe, baada ya bwana Sese kumpiga sana akamwambia,
“Aisha usiposema hii mimba ni ya nani mimi nitakuua leo, mimi sina uwezo kabisa wa kumpatia mwanamke mimba” bwana Sese huku akitoa machozi alisema, kisha akaendelea
“Mwaka jana nilivyopata ile ajali ya pikipiki nikalazwa wiki tatu hospitali, kuna siku dokta alinifuata wodini akaniambia, kwa situation ya ajali kuna sehemu za mfumo wangu wa uzazi ndani ya mwili hazitofanya kazi tena, kwahiyo sintokuwa na uwezo wa kumpatia mwanamke mimba, niliumia sana kiukweli sikutaka nikupoteze katika maisha yangu, na kwasababu tulikuwa katika uchumba nikaamua kuliweka moyoni ila nilipanga nitakapo kuoa siku moja ningekueleza, kwahiyo naomba uniambie tu ukweli hii mimba ni ya nani” alimaliza bwana Sese huku muda huo machozi yamemfika shingoni.
“Nisamehe mume wangu, ni shetani tu alinipita, hii mimba ni ya D..a.n..i..e.l, JIRANI CHUMBA CHA PILI” Aisha akatoboa kwa kigugumizi.
Bwana sese akakunja ndita akapandwa na hasira mara dufu, alimfahamu vyema jirani yake huyo kwani tangu amehamia hapo amekuwa ni mtu wa kubadilisha wanawake kila kukicha, akajua ni dhahili alimlagai mke wake, akaapa mbele ya mke wake,
“I swear! huyu ny’angau leo namuua kama amezoea kuchezea wanawake wapumbavu pumbavu basi leo ndo mwisho wake, hapa ameingia Jehanamu” akafungua mlango kwa hasira kisha akaondoka.
********
Daniel hakutaka kuonesha chochote mbele ya Mhudumu akasubiri aondoke kisha akamuuliza Sarah Mwakalinga,
“Mbona chumbani tena, kwani hapa hatuwezi kuongelea hayo maongezi?
“Hapa nje hapafai Daniel, kuna watu wanapita pita wananifahamu, kwahiyo inakuwa haipendezi we twende tu haina shida tutaongea kwa muda mfupi kisha tutaondoka”akajaribu kumshawishi.
Daniel hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali, Sarah mwakalinga mbele Daniel nyuma, Daniel akawa anamtizama mama huyo mavazi aliyokuwa amevaa yalimbana kiasi na kufanya maungo yake ya nyuma yajichonge vema, lakini akayatupilia mbali mawazo yake kutokana na umri wa mama huyo kusogea.
Walipota eneo hilo la garden kuelekea ndani kuna binti alikuwa kakaa kando yao akavuta simu yake akapiga kisha akasema,
“Wametoka garden sasa wanaenda ndani, nadhani wanaelekea chumbani”
“Basi fuatilia Chumba watakacho ingia ila hakikisha hawajakushtukia” upande wa pili ukasikika sauti ya mwanaume ikizungumza kwa kukwaruza,
“Sawa boss” akajibu yule binti.
Previous Post
Next Post

0 Comments: