Monday, November 11, 2019

JIRANI, CHUMBA CHA PILI (06).

MTUNZI: AMMI CYPHER
AGE…(18+)
Ilipoishia…
“DANIEL MHENGILOLO” aliita yule mama
Daniel akashtuka mno, ni vipi mama yule amelifahamu jina lake ilihali ndo mara ya kwanza anamuona mama yule
ENDELEA NAYO:
“Mbona umeshtuka hivyo vipi kwani siyo jina lako?”
“Ni jina langu ila ni vile nimeshangaa tu sikufahamu kabisa” Daniel muda huo alikuwa ashatosheka na ashasafisha mikono, muda huo yuko na tishu anajikausha kuianza safari ya kuondoka, basi mama yule akatoa business card yake akampatia kisha akasema,
“Ukipata time nitafute, tutaongea kwa kirefu zaidi”
Daniel akaaga akaondoka eneo hilo huku akiwa na mawazo lukuki juu ya mama huyo.
***********
Mchezo wa Aisha ulikuwa ni ule ule kila siku usiku ilikuwa ni lazima amtoroke mumewe bwana Sese na kwenda kurusha roho kwa Daniel, mchezo ukawanogea.
Siku hiyo baada ya kuamka asubuhi, Aisha akajikuta hali yake haielewi elewi kabisa kengele ya hatari ikagonga kichwani mwake akaomba mungu anachokiwaza kiwe tofauti na akili yake inavomwambia, akatoka nje akanyoosha mpaka lilipo duka la madawa, akanunua kipimo kisha huyo akanyosha mpaka chumbani kwake, akaingia chooni akachutama akafuata njia zote zinazopaswa akasubiri baada ya dakika tano akakiinua kile kipimo, majibu ya kile kipimo yalimshtua kupita maelezo, alikuwa ni mjamzito na kumbukumbu zake zinamthibitishia ujauzito huo ni wa Daniel, katika starehe zao zote ambazo wamewahi kufanya hawakuwahi kutumia mpira na katika kila mchezo Daniel amekuwa akimwagia ndani, na tangu Daniel amehamia hapo amelala naye mara nyingi kuliko alivyolala na mume wake.
“Mungu wangu hii dhambi gani tena, Unyama gani huu nimemfanyia Sese, hivi ni kweli nimeshindwa kabisa kuilinda ndoa yangu, na vipi Daniel atalipokeaje swala hili” alizidi kujiwazia Aisha, maji yalikwisha mfika shingoni,
“Ila siyo mbaya Daniel akiikataa nitasema ni ya Sese mimi mtoto wa mjini, haya mambo madogo sana kwangu” alijishauri.
*******
Sara Mwakalinga, Manager wa TRA mkoa wa iringa baada ya kusikia sifa za Daniel Mhengilolo kutoka kwa shosti yake Asia ambae pia ni mfanyakazi mwenzake akajikuta amevutiwa na mwanaume huyo ambaye hakujua hata anafananaje,
“Kwahiyo Asia unataka kusema huyo mwanaume ni hatari sana mkiwa kwenye sita kwa sita? Aliuliza Sara mwanamama ambaye umri wake umekwenda lakini yeye amegoma kabisa kwenda, anajikuta kwenye mchecheto baada ya kuzisikia sifa za Daniel,
“Shosti usipime kabisaaa ana ufundi ambao hujawahi kuuona sehemu nyingine, walah pale nayafaidi mautamu mapenzi ninayompa sidhani kama anaweza kuingia kwenye mahusiano na mtoto yeyote wa chuo”
“Heeeh! Asia kumbe ni mtoto chuo” Sarah Mwakalina akauliza kwa kushangaa
“Hapana shosti ni lecture hapo mbele chuo cha Rucu, Mi mtoto wa chuo nampeleka wapi hahah ha!! embu ngoja nikuoneshe picha zake jinsi alivyo gentleman” akatoa simu yake akaingia kwenye galley akaanza kumuonesha shosti yake picha baada ya picha, Sara mwakalinga akajikuta amevutiwa na kijana huyo akaapa kwa namna yoyote ni lazima amzunguke shosti yake huyo ili na yeye ayaonje hayo ambayo amekua akiyasikia kutoka kwa asia.
Ndio maana ikawa kila lunch anaenda kula kwenye Restaurant zilizo karibu na chuo, nia na kusudi ni kumnasa Daniel, Na hilo akafanikiwa siku hiyo baada ya kumkuta Daniel anapata lunch, kumpatia business card yake akaamini hilo ni goli la kwanza amefunga.
*********
Ni katika Luxury pub maeneo ya ccm mkoa Daniel akiwa na Mshkaji wake Barnabas mwakalukwa, mshkaji ambaye walisoma wote advance level na elimu ya chuo pamoja wakilainisha koo zao,
“Daniel unajua wewe sasa siyo mshkaji wangu tena ila ni zaidi ya ndugu yangu wa damu? Alianza Barnabas mwakalukwa baada ya kuwa eneo hilo zaidi ya lisaa,
“Ni kweli kabisa unalolisema kaka, ila kwa muonekano wako nahisi kuna jambo unataka kulisema mana nakuelewa wewe ni mtu wa falsafa tangu tukiwa A level” akajibu Daniel ukirudisha glass ya wine kwenye meza baada ya kupiga kumeza funda,
“Ndiyo Danny kuna jambo limekua likinitatiza sana katika kichwa changu kuhusu wewe, Huu ni mwaka wa tatu tangu umepata ajira pale chuo, lakini katika miaka hiyo mitatu mzee sijaona maendeleo yoyote ambayo umeyafanya, labda umenunua shamba au umenunua kiwanja unataka kujenga, we kila siku umekuwa ni mtu wa kuhama hama tu magheto, leo ilala, kesho gangilonga, mala upo ipogoro leo pale miyomboni unataka kuhama wakati hata miezi mitatu hujamaliza kaka wewe umri unasogea unatakiwa uwe na assets kama hizo we ni msomi lakini mambo yako huyaendeshi katika engo hizo”
“Hahaah ha! kaka yani katika maisha yangu tangu nimekufahamu hakuna siku tumewahi kukaa siku hiyo ikapita hivyo bila kunishauri jambo, lakini ni vizuri wewe ni rafiki mzuri ambaye hupendi kuona ndugu yangu ninapotea, lakini kaka katika vitu sijawahi kufikiria katika maisha yangu ni pamoja na kujenga, kaka kujenga ni uoga wa maisha, niamini mimi” aliongea daniel kwa sauti ya kilevi huku hali yake inaonesha tayari pombe imemkolea,
“Kaka embu muone yule waiter anaehudumia kwenye ile meza pale kwenye kona, cheki mtoto lile shepu lilivo makini, yule mtoto lazima nitoke nae hapa, hakiiiiiii yaaaa mungu! Akaapia Daniel huku akitoka kwenye mada ambayo rafiki yake alikuwa ameianzisha. Barnabas mwakalukwa akabaki anasikitika akaanza jitihada za kumtoa mshkaji wake eneo hilo ili waondoke amrudishe anakoishi.
***********
“Kwani hayo ni maongezi ya aina gani mpaka tukaongelee hotelini mama? Daniel simu ikiwa sikioni siku hiyo anaongea na Sarah mwakalinga akiwa na shauku ya kutaka kujua ni vipi mama huyo aliifahamu jina lake na alikuwa anataka kujua ana mazungumzo gani na yeye,
“Ni maongezi ya kawaida tu daniel sema yenye uzito kidogo, pia nataka tukaongee kwenye sehemu iliyotulia sitaki kwenye sehemu changanyikeni”
“Sawa nambie hiyo venue mama”
”Pale Saivilla nadhani ni poa sana, si unapafahamu?
“Mmmh mmh ndiyo ndiyo napafahamu” alijibu Daniel kwa kigugumizi siyo kwamba alikuwa anaifikiria sehemu hiyo kwamba anaifahamu au aifahamu, hapana ni kutokana na uzito wa sehemu hiyo amekuwa akipitaga tu na kwa taarifa ambazo amewahi kuzisikia ni kwamba hoteli hiyo huwa inatumiwa na mawaziri wakubwa wakubwa pindi wawapo mkoani iringa na gharama ya chumba cha kima cha chini aliwahi kusikia ni laki sita.
“Sawa utanikuta hapa, ukifika utanipigia”
Daniel akajiweka sawa akatoka nje ya nyumba anayoishi akaita bodaboda, akamuelekeza anapoelekea, kisha safari ikaanza.
“Nimefika nipo hapa reception” Daniel baada ya kufika hotelini hapo alimpigia Sarah mwakalinga
“Sawa mwambie huyo dada akulete huu upande wa Saadani park, nimekaa hapa”
Baada ya sekunde kadhaa Daniel akafikishwa hapo saadani park, ni bustani iliyopangiliwa ikapangika, Daniel pamoja na kuwa ni mtu wa viwanja lakini hoteli hiyo amekuwa akiisikiaga kwa watu ambao waliwahi kubahatika kufika hapo, akabaki anashangaa shangaa tu kama mwizi aliyefika kwenye nyumba ya tajiri na kukuta vitu vingi vya thamani na hajui aanze kuiba kipi aache kipi.
“Shkamoo mama, vipi sijakuchelewesha sana” Daniel alianza kwa salamu huku akivuta kiti na kuketi
“Niko poa Daniel, hizo shkamoo zako ni salamu za kizamani sana zimepitwa na wakati sikuhizi. But anyway nimefurahia ujio wako”
“Sawa mama, okay nambie hayo maongezi uliyosema yana uzito kidogo”
“Daniel una haraka mno, mambo mazuri hayataki haraka, sorry Mhudumu!
“Naam naomba kuwasikiliza” alisema mhudumu baada ya kufika mezani hapo
“Naomba umsikilize mwenzangu hapo, kisha atakachoagiza utatuleta chumba cha Sokoine pale”
Sarah Mwakalinga akamwambia mhudumu, Daniel akaonekana kushtuka baada ya kusikia habari za chumba. Kisha akasema,
“Naomba short ya taquira”
Previous Post
Next Post

0 Comments: