Monday, November 11, 2019

JIRANI, CHUMBA CHA PILI (03).


EPSD 03
MTUNZI: AMMI CYPHER
AGE…(18+)
Ilipoishia…
Wakiwa katika ya penzi mlango wa Daniel ukagongwa, akashtuka kwa sababu hakuna mtu mwingine zaidi ya Rose ambaye anafahamu anapoishi.
ENDELEA NAYO:
Akajitoa mwilini mwa Rose akafikiri kidogo kwamba ni nani ambaye anaweza kuwa anagonga, mwishowe akakata shauri akaenda bafuni akachukua tauro na kwenda kufungua mlango akakutana uso kwa uso na Dada mmoja mrembo,
“Samahani kaka kama nitakua nimekusumbua mi naitwa Aisha naishi hiki chumba cha pili kinachofuata kutoka kwako, mimi ndiye huwa nasimamia hii nyumba, Samahani jana wakati unafika hatukuonana ila nilipigiwa tu simu na mwenye nyumba kwamba kuna mpangaji mpya angefika jana, kwahiyo nilitaka nikupe utaratibu kidogo wa nyumba yetu hii” alisema dada huyo aliyejitambulisha kwa jina la Aisha
“Sawa nakusikiliza”
“Hapa kwetu utaratibu wa umeme ni elfu 10 kila unapokata, bili ya maji itategemeana na matumizi yetu yalikuaje, lakini la mwisho ni utaratibu wa usafi. Hapa kwetu kila mpangaji anachoo chake cha ndani hilo halina shida ila kwa hapa uwani kuna ka mchango kidogo ambako tunamlipa mfanya usafi ambako ni elfu tatu kwa mwezi, na Kuna ndoo ya taka pale mlango wa kutoka nje kwahiyo ukifanya usafi ndani kwako au mabaki ya chakula utakuwa unatupa mule kisha mfanya usafi atakuwa anaenda kutupa dampo, Ni hayo tu kaka yangu nisamehe kwa kukuamsha naona macho mekundu ulikuwa umelala” alisema Aisha huku akitabasamu.
“Usijali”
akajibu Daniel huku akirudi ndani kwa mpenzi wake akachukua simu yake akakuta missed call tatu kutoka kwa Betty akatupa simu pembeni kisha akamgeukia Rose
“Baby tukaoge mana nimechoka hatari”
“Mimi pia nilikua na wazo hilo ila ni vile tu umeniwahi”
*******
Betty baada ya kumpigia simu Daniel akawa hapokei alichukia sana akaamua kujiandaa, akachukua funguo za gari yake na kutoka. Safari yake ikaishia 255 pub, akazima gari yake akapandisha vioo akaweka kimini chake vizuri kisha akashuka kwenye gari kwa mwendo wa malingo akaingia mpaka ndani.
Akanyosha mpaka sehemu yenye kigiza cha wastani akavuta kiti akaketi, sekunde kadhaa mhudumu akamfata,
“Karibu dada naomba nikuhudumie”
“Naomba grants ya kati, naomba uniletee na ndimu pia”
“Sawa haina shida”
Baada ya kupiga glass kadhaa na muda ulikwisha kwenda akajikokota kuinuka kwenye kiti huku akiyumba alikuwa kazidisha kipimo chake cha kunywa hakuwahi kunywa glass nyingi kama siku hiyo, akajivuta mpaka nje alipokaribia gari yake akajikuta anatapika watoto wa mjini wanaita kurudisha chenji akatulia kwa sekunde kadhaa akawa haoni vizuri kila akitaka kuchomeka funguo kwenye kitasa cha gari akawa anaona vitasa viwili.
Kwa bahati kuna lecture alikua kwenye pub ile pia, akaiona gari ya Betty akasogea pale walau ampe hai, akamkuta Betty kaegemea gari kapitiwa na usingizi funguo imeanguka chini haelewi kitu, akajaribu kumsemesha lakini Betty alikuwa kimya akaokota funguo akafungua mlango akampakia kisha akawasha usukani, akajaribu kumtikisa walau amuulize anapoishi ampeleke lakini ndo kwanza Betty alizidi kukoroma.
Jinsi Betty alivyokuwa amelala kihasara kwenye siti akajikuta anajigeuza geuza kitu kilichopelekea kimini chake kupanda kwa juu kidogo, Lecture akiwa anafikiria sehemu ya kumpeleka Betty kwa wakati huo, alipomtazama Betty akaona jinsi kimini kilivyopanda kwa juu nguo ya ndani inaonekana, akamtazama jinsi mapaja yake yalivyonona, akajikuta pepo la ngono limemuingia hapo hapo akakata shauri na kumpeleka kwake kwakuwa anaishi mwenyewe na ni muda mrefu amekuwaga akimtamani mwanamke huyo.
Walipofika kwake akamshusha kutoka kwenye gari akamuongoza mpaka ndani akamkokota hadi chumbani huko akambwaga kitandani akamvua nguo zote akabaki mtupu, akamtazama kwa sekunde kama tano hivi akawa haamini kama kweli amemnasa mwanamke huyo ambae amekuaga akimtamani siku zote pale kazini, wote ni ma lecture wa chuo cha Rucu isipokuwa wako department tofauti yeye akiwa department ya Social science na Betty akiwa Computer science.
“Hatimae leo mbuzi kafia kwa muuza supu” alisema huku akianza kuvua nguo zake tayari kuanza mtanange wa bila refa.
********
Daniel akiwa anaingia kazini kichwani akaanza kufikiria jinsi jana alivyopata vitu adimu kabisa kutoka kwa Rose
“Ila Yule mtoto ni mtamu siyo siri, kwa hali hii wallah! nitajikuta sijengi katika maisha yangu” alisema huku akijikuna kichwa.
Lakini akiwa amekaribia mlango wa kuingia ofisini akasimama akafikiri kwa muda ni jinsi gani atampanga Betty amuelewe ni kwanini hakupokea simu yake na walikuwa na miadi ya kukutana jana,
“Ila mimi ni mwanaume naweza kum-hendo, sijui kwanini naumiza kichwa”
Kwa bahati alivyoingia ofisini alipotupa macho yake kwenye meza ya Betty hakumuona akajua ni lazima atakua kwenye kipindi akanyosha mpaka kwenye meza yake akaketi akachukua simu yake akaandika meseji,
ROSE VIPI BADO UMELALA? Kisha akatuma
HAPANA BABY, HAPA NILIKUA NAJIANDAA NDO NATOKA HIVI FUNGUO SI NAKULETEA HUKO CHUO? Rose alirudisha sms
NO UTANIWEKEA TU HAPO JUU YA MLANGO. Hakutaka chuoni aonekane ana ukaribu na mwanamke yoyote hivo alihofia kupeperusha ndege wake wengine. Akaiweka simu yake pembeni tayari kuianza siku mpya chuoni hapo.
**********
Betty anaamka asubuhi na kujikuta kwenye mazingira mageni kabisa, anaangaza huku na huku kwenye kuta za chumba hicho anabaki anashangaa amefikaje hapo anakumbuka mara ya mwisho alikua pub 255 lakini hakumbuki kingine tena kilichoendelea, anageuza macho pembeni yake anaona kuna mtu amelala lakini kajifunika mpaka kichwani akashtuka, akajichungulia kwenye shuka akajikuta yuko kama alivyozaliwa, huku kwa mbali akihisi maumivu kwenye ikulu yake,
“Hivi ni nini kiliendelea pale 255” aliwaza Betty

Previous Post
Next Post

0 Comments: