Monday, November 11, 2019

NAMNA YA KUACHANA NA MTU AMBAYE BADO UNAMPENDA/KUPUNGUZA MAUMIVU BAADA YA KUACHIKA!

Taswira inaweza kujumuisha: mtu mmoja au zaidi
Watu wanapoanzisha mahusiano hufanya hivyo wakiwaza kuishi milele, mahusiano yana changamoto zake, nivizuri kuangalia namna ya kuzitatua kabla ya kuwaza kuachana. Lakini kuna wakati mwingine katika mahusiano unaona ni bora na ni vyema kwako kuachana na mwenza wako hasa kama unaona mambo hayaendi sawa, ushajaribu kila kitu lakini haiwezekani.
Kuna aina ya mahusiano mengine ukiangalia unaona kabisa ushaachana na mhusika na umeshikilia tu kwakua bado una matumaini labda atabadilika, labda mambo yatakua sawa au kwakua tu una maumivu. Makala hii naiandika kwaajili ya kumjibu mteja wa kitabu changu ambaye anaumia kutokana na kuwa mtu anayempenda hamjali na amefanya kila kitu lakini imeshindikana.
Ndiyo kama unaona mahusiano yenu hayaendi popote, kila siku mnagombana kuhusu kitu kile kile au mwenza wako hakujali kabisa unaona anakutumia tu, hata kama unampenda vipi kwa afya ya moyo wako nivyema kuondoka. Siwezi kukuambia kua itakua rahisi, kukuambia kua hutaumia, hapana ni ngumu kama kweli ulikua unampenda na utaumia kweli lakini mbinu zifuatazo zitakusiadia kupunguza maumivu.
(1) Kumbuka Kuwa Huwezi Ku Control Kila Kitu; Mapenzi ni ya watu wawili, hivyo ili yafanikiwe nilazima wote muwe katika ukurasa mmoja, wewe unapotimiza majukumu yako unakua umefanya kila kitu, lakini kwabahati mbaya sana nikuwa huwezi kucontrol kila kitu, kwamba huwezi kuulazimisha moyo wake, huwezi kumlazimisha kuwa kama unavyotaka, huwezi kumfanya kuwa mwema na kubwa kabisa huwezi kumfanya akupenda kama moyo wake hautaki.
Chukulia mapenzi kama mvua, huwezi kucontrol mvua kunyesha, kuwaka kwa jua na vitu kama hivyo. Hapa namaanisha kuwa, ingawa wakati mwingine utajisikia vibaya, utajilaumu na kuona kama labda ulikosea sehemu, utawaza laiti ningefanya kitu flani na kuwaza sana, wakati mwingine si wewe, kama haiwezekani haiwezekani tu. Wewe si Mungu hivyo hembu unapoamua kumuacha kaa chini na angalia je umefanya vyakutosha, je umeonyesha mapenzi yako yote.
Lakini inawezekana labda wewe ndiyo ulimkosea, jiulize je umemuomba msamaha, je umebadilika kwa dhati kabisa. Kama umefanya hivyo vyote basi sasa unaweza kusema ni Mungu alipanga, hili liko nnje ya uwezo wangu na ni bora kuachana kuliko kuendelea kuumia. Acha kulazimishia tena, acha kujipa matumaini tena, kubaliana na hali halisi na fanya maamuzi, si kosa lako, huwezi ku control kila kitu na hiki ni moja wapo ya ambavyo huwezi kucontrol.
(2) Mambo Yatakua Mabaya Zaidi/Utapoteza Muda Zaidi; Najua Bado unawaza, kuna kumbukumbu nyingi nzuri ambazo mlipitia, lakini sasa ni kumbukumbu, yamebaki magumu tu na haya ndiyo hukuumiza. Lakini pia unawaza kuhusu muda, umetumia muda mwingi sana kwa huyu mtu, umetumia pesa nyingi na hata kuna mambo mengi ambayo umejitoa kwake, hata kazi uliamua kaucha au hata mliwekeza pamoja.
Unaona ugumu kumuacha ukiwaza vitu ulivyopoteza, labda nikuambie tu, kuwa kila sekunde unayoendelea kuwa naye unazidi kupoteza zaidi kupoteza muda zaidi, unazidi kujirudisha nyuma. Kuna hatua ambayo hata wewe unaona kuwa hatabadilika, hivyo badala ya kaungalia vitu ulivyopoteza hembu angalia kumbukumbu nzuri kutoka kwake. Kuna mambo mengi mazuri ambayo mlifanya pamoja, yachukue hayo na yale mabaya, muda uliopoteza na kila kitu ulichopoteza muachie yeye na jua kua ni sehemu ya maisha.
Usipoteze muda mwingine wa zaidi kwake, acha kujishusha zaidi, acha kunyenyekea zaidi. Kuendelea naye ukiwa na matumaini labdda mambo yatabadilika wakati huoni dalili, au ashakuambia tayari kuwa hakutaki tena, ashakuonyesha kuwa na mtu mwingine lakini bado una ng’ang’ania, huna furaha lakini bado unashikilia muda uliopoteza basi utazidi kupoteza zaidi, kubali yaishe, sema imetosha na anza upya.
(3) Fanya Maamuzi Ya Kwako Na Muambie Kuhusu Maamuzi Yako; Sasa inawezekana bado mnawasiliana, hajakuacha rasmi, anasema kua bado nakupenda lakini haishi kukuumiza kila siku, umechoka! Lakini inawezekana kashakuambia hakutaki, kashakuambia kua hawezi kuwa na wewe na hataki hata kukuoana, labda ana mtu mpya sasa. Lakini ukishaamua kua humtaki tena, unaendelea na maisha yako, hembu hakikisha unamuambia, ajue kua umeamua kumaucha.
Ndiyo hata kama ameshakuacha, kumbuka kama kakuambia sikutaki ni yeye alikuacha lakini wewe ulikua bado hujamuacha, hivyo mtafute iwe ni kwa simu, kwa kuoanana au hata kwa meseji, muambie yote ambayo ungetamani kumuambia, namna ulivyoumia na kisha muambie huwezi kuendelea naye tena na sasa unaondoka huwezi kugeuka nyuma.
Nakuambia ufanye hivyo kwa sababu, na hili ni muhimu. Kuachana na mtu unayempenda ni tofauti na kuachana na mtu wa kawaida, mara nyingi watu huachana huku wakiwa na matumaini kuwa labda atarudi, hata kama washaachwa na kuambiwa sasa ili ujisikie vizuri na ujishawishi kukubaliana na ukweli kuwa ushaachana naye nilazima wewe utamke, umuambie kuwa ushaachana naye. Hili ni la muhimu sana katika kukusaidia kuendele ana maisha yako.
(4) Acha Kuingia Kwenye Mchezo Wa Kuombana Misamaha; Hii ipo mara nyingi sana kwa Dada zangu, unapomuambia mwanaume nimekuacha, au mwanaume akikuacha anaona kama utarudi tu, tena hasa mkishatumia muda mrefu kwenye mahusiano. Hivyo ukimuambia umeachana naye anajua kua unatania, nakuacha na kukupotezea baada ya wiki mbili anaona uko siriasi anakutafuta.
Anaomba msamaha wewe na wewe ukiangalia muda ambao mmepoteza unaona poteli ya mbali unamsamehe. Lakini ni mwezi mmoja tu anarudi kulekule, kisha unamucha tena natena natena. Dada yangu ukishaamua kuachana na mtu, sisemi kua hakuna kusamehe lakini hembu jiuliza unasamehe kabadilika kweli au anakuambia atabadilika. Mtu umemuacha wiki anajifanya kabdailika, hapana!
Kama ukiamua kauchana na mtu, hasa ambaye amekuumiza kwa muda mrefu, ambaye unaona kabisa hawezi kubadilika, amua kweli na usigeuke nyuma ukaingia katika mchezo wa kuachwa na kuomba msamaha. Labda kwa kukusaidia zaidi nikuwa kama umemsamehe mara ya kwanza kosa lile lile, karudia ya pili kosa lilelile ukimsamehe ya tatu basi wewe ndiyo mwenye matatizo kwani habadiliki huyo, hivyo kusamehe si vibaya lakini si kusamehe kila siku anakuchukulia poa huyo.
(5) Jiruhusu Kuumia; Ndiyo ni mtu ambaye unampenda, kuna mambo mengi ambayo mlishea hivyo usidhani utamaucha tu na kisha kila kitu kikaa sawa, hapana kuna kitu kinaitwa maumivu na utaumia sana tu. Jiruhusu kuumia, usiachane naya na kukaa na kitu rohoni, unaweza kulia kama ni mtu wa kulia, ukaongea na marafiki, ukaongea na watu wa karibu, jiruhusu kua na hasira kuomboleza na kufanya kila kitu mbacho kinakutoa hasira.
Hutamsahau kwa haraka kihivyo, usijali ni kawaida, nilazima uomboleze. Lakini fanya hivyo ukijua kuwa huo sio mwisho wa maisha, ulikua na furaha kabla yake na sasa utakua na furaha tena baada yake. Hilo ni jambo ambalo unapaswa kuliweka kichwani, jua kuwa maumivu uliyonayo sasa si ya kudumu, ni ya muda na kidonda kitapona hivyo wakati ukijiruhusu kuumia kwa muda waza kuhusu furaha ambayo inakungoja mbeleni.
(6) Futa Kumbukumbu Zake/Mkwepe; Kuna wale watu ambao wanasema kua tuachane lakini tuendelee kua marafiki, hakuna kitu kama hicho, kama unaona kuwa umechana na mtu na bado ni rafiki yako basi jua mlikua hampendani kihivyo au bado hamjaachana, mmesitisha tu mahusiano. Nilazima ujifunze kumsahau na fanya hivyo kwa kuondoa kumbukumbu zake, achana na kila kitu ambacho kinakukumbusha kuhusu yeye.
Futa namba zake za simu na unaweza hata kumblock kwenye mitandao ya kijamii, unajiumiza tu na hutamsahau kama kila siku unaingia kwenye akaunti zake kaungalia kampost nani, nani kalike, nani kacomment, je anafuraha? Kama unamfuatilia mpenzi wake mpya, kujua kama anafuraha, kama ni mzuri kuliko wewe na kila kitu, huko si kauchana huko nikuwa mlinzi wake. Acha kutafuta sababu ya kuoanana naye na kutaka kujua kuwa anaendeleaje ni kujitengenezea maumivu tu!
(7) Usiingie Kwenye Mahusiano Mengine Ili Kumsahau; Kila mtu ana muda wake wa kumsahau mtu, muda wa kuomboleza, kuna ambao wanaachana leo na kesho wako sawa tu. Lakini kama wewe ni wale wa kupenda sana na ulikua unapenda kweli basi hembu jipe muda wa pake yako, muda wa kutafakari kuhusu maisha yako kuliko kuingia kwenye mahusiano mapya.
Huwezi kumsahau kwa kuingia katika mahusiano mapya, lakini pia haitakua sahihi kwako na kwa yule ambaye unaingia naye katika mahusiano. Hivyo unapoachana na mtu, usirudi kwa kuangalia mtua maybe alishakutongoza au anayekutongoza, kuangalia mtu ambaye ulishamtongoza kuwa ndiyo umfuate, hapana hembu jipe muda wa kuomboleza, kuwaza maisha yako na kufanya mambo yako kabla ya kuingia kwenye mahusiano mengine.
(8) Tafuta Sehemu Ya Kuelekeza Akili Yako; Unaumia sana kwakua unatumia muda mwingi sana kumuwaza. Hembu sasa tafuta kitu cha kufanya zaidi, wekeza akili yako huko, inaweza kuwa ni kazi, mradi mpya, biashara mpya au kitu kingine kipya. Lakini inaweza kuwa ni hobi au kitu kingine kile, tafuta kitu cha kukuchukullia mudua wako, kitu cha kukufanya usiwe poeke yako, toka na marafiki, fanya mambo mapya, usiiache akili yako ikawa wazi, angalia movie au tengeneza kitu cha kukufanya bize tu.
(9) Kuna Mambo Mazuri Yanakuja Mbele Yako; Watu wengi hudhani kuwa wanapoachana na watu waliokua wakiwapenda sana ndiyo unakua mwisho wa maisha yao. Kwamba hawatakua na furaha tena kwakua walishawahi kuwa na furaha. Hii si kweli, unapaswa kujua kua furaha yako unatengeneza wewe mwenyewe na ni jambo la kimaamuzi kama uhusiano unaofuata uwe ni wa maumivu au la?
Kama safari hii ilishindikana kua na furaha basi jua kuwa kuna mlango mwingine ambao unapaswa kuufungua ili kuwa na furaha. Kuna sababu mmechana na Mungu ana mipango mingi sana na wewe hivyo badala ya kukaa ukilia, ukaomboleza hembu mshukuru Mungu kuwa kakuonyesha huyo ni mtu wa aina gani na kuna furaha nyingine mbele inakusubiri.
(10) Acha Kuendelea Kuomboleza Na Kujionea Huruma; Mwisho wa mahusiano ya mateso ndiyo mwanzo wa mahusiano ya furaha. Kama umeamua au unaona kuwa nilazima uachane naye, kama ushaachana na mhusika na bado unaumia, hembu rudia makala hii, anza kufanya jambo moja baada ya jingine halafu utaona matokeo yake baada ya muda flani, si kitu cha siku moja, umekua kwenye mahusiano na huyo mtu kwa muda mrefu itachukua muda.
Previous Post
Next Post

0 Comments: