Tuesday, October 29, 2019

CHOMBEZO:HOUSEGIRL WA DADA.

Image may contain: 2 people, people sitting and text
EPISODE 03
ILIPOISHIA.
Nilipata wazo la kuamka na kwenda kufungua mlango wa chumba cha Alice nilivyosukuma bahati nzuri mlango ulikuwa haujafungwa niliingia moja kwa moja chumbani kwake na kuwasha taa.
Nilichokikuta chumbani kwake sitoweza kusahau kamwe .
ENDELEA SASA.
nilikuta kibuyu kiko kitandani kimefungwa vitu vya rangi tofauti kama hilizi na vitambaa vitatu vya rangi tofauti cheusi, nyekundu na nyeupe.
Vilikuwa vimetandikwa kitandani kwa Alice nilivyoona vibuyu na hali ilivyokuwa mle chumbani kwake niliogopa sana na jasho lilianza kunitoka maana nilijua moja kwa moja Aliice ni mchawi na muwangaji maana sikumkuta chumbani kwake.
Wakati bado nazubaa nilitaka kufungua mlango na kutoka nje gafla Alice alitokea akiwa ameshika mtoto mdogo sana alikuwa amebadilika na kuwa na sura nyingine .
Aiseeee nilianguka chini na kuita dadaa, kwa ajili ya msaada lakini hawakuweza kunisikia maana sauti ilikuwa haitoki, nilifungua mlango na kutaka kutoka chumbani kwake lakini Alice aliufunga kimiujiza na sikuweza kuufungua ule mlango nilibaki mle chumbani kwake nikiwa nimelowa jasho mwili mzima.
Alice alianza kucheka kwa cheko la kichawi ahaaaa ha aha ahahaaaa haaaa ha huku akinizunguka akiwa na yule mtoto mdogo alinipiga na mkia aliokuwa ameushika hapo sikuweza kujua niko wapi nilihisi nasafirishwa kutoka pale nilipo na kuelekea kuzimu.
baada ya kupigwa na ule mkia kichwani na kunizunguka Mara tatu niliweza kuhisi nasafilishwa kutoka sehemu ile na kuelekea sehemu nyingine ambayo nilikuwa siijui na nilikuwa sijitambui nilikuwa napelekwa tu, nilikuwa nahisi tunazama kwenda chini.
Tulifika sehemu niliona geti likifunguliwa tuliingia ndani humo kulikuwa na watu wengi sana na walikuwa wa aina tofautitofauti kiasi kwamba sikuweza kuwatambua niliweza kusilka tu sauti zao “mlete huku, mlete huku” Alice kwa muda huo alikuwa bado amemshikilia mtoto yule.
Lakin baada ya muda kidogo alikuja bibi mmoja mzee sana ambaye alivalia mavazi meusi na mekundu na kusema mchukue huyu na mlete huku, Alice alinipeleka hadi chumba kile, wakati naingia chumbani kwa bibi ulivumaa upepo wa ajabu sana sikuweza kujua tena tumepitia wapi na nitatokea wapi maana chumba kile kilikuwa kama yai na mimi nilijiona niko ndani ya yai ambalo halina mlango wala dirisha, kwa muda huo niliachwa peke yangu, Aice alikuwa ameshaondoka zake.
Bibi aliingia tena na sikujua anetokea wapi mle ndani kwa muda ule sikuona kiti cha kukalia wala meza lakin Mara baada ya bibi kuingia alibonyeza tu sehemu moja ukutani na viti vikaja na niliambiwa nikae kwenye kiti kile.
Bibi kizee alianza kuniambia “umezini na mwanangu inamanisha anakupenda na unampenda hivyo yakupasa ukubaliane na masharti ya huku kwetu na huyo ndio atakae kuwa mkeo maana anakupenda, na huku kwetu kazi yetu kubwa ni kutafuta watoto wachanga kuchukua damu zao kuanzia sasa utakuwa katika jukumu la kuzunguka mahospitalini na kuchukua watoto wachanga sawaaaaaaaa” aliongea huku amenikazia macho na alikuwa anabadilikabadilika kiufupi alikuwa hana umbo maalumu kwa upande wangu sikuweza kujitambua na masharti yale niliona magumu kwangu nilimuwekea ngumu kukubali kuweza kua!
Tulibishana pale na yule bibi kwa dakika kadhaa na alivyoona nimemzidi aliniziba mdomo na sikuweza kuongea tena kwa muda ule nilikaa kimya na alianza kunipaka vitu vyake na kuniambia binti yangu anakupenda na ole wako useme kuwa ni mchawi nitakuua.
Alimaliza kuongea aliweza kunyoosha mkono na mlango ulionekana nilichukuliwa kama upepo kutoka mle ndani aiseee usiku huo sikuweza kulala nyumbani kabisa yani baada ya kutolewa mle ndani nilipelekwa sehemu ya kutolea adhabu na sehemu ya kutunzia damu duuuuuuu damu zilikuwa nyingi sana na sehemu ya adhabu alikuwepo nyoka mkubwa mno.
Nilizungushwa maeneo mengi huku bado nikiwa bubu siongei chochote muda wa kurudi duniani uliwadia maana asubuhi ilikuwa imekaribia kwenye saa kumi moja asubuhi.
Alice alirudi na kunichukua hadi nyumbani tulitokezea chumbani kwake palepale aliponipigia mkia wake, alinipiga tena mkia wake ule kichwani maraa tatu na kunizunguka.
Hapo akili ilirudi na niliweza kujitambua nilikurupuka na kumuangalia Alice alininyoshea kidole na kusema “usiropoke chochote kwa Dada yako au kwa mtu yeyote nitakuua Mara moja ” aliongea hivo macho yake yalikuwa yamebadilika na kuwa kama ya paka yaani yalibadilikabadilika na kuwa rangi tofauti tofauti!
Aliweza kufungua mlango wake kwa nguvu zake za giza, ulifunguka na nilitoka nakimbia kuelekea chumbani kwangu nilimuogopa sana Alice kuanzia siku hio maana alikuwa sio binadamu wa kawaida nilanza kukaa nae mbali.
Lakini yeye aliona kawaida sana, hapo nyumbani niliwaza hivi dada yangu anajua hii hali ya Alice kuwa sio mtu mzuri niliwaza kumwambia lakini nilihofia usalama wangu maana bibi yule kule tulikoenda alisema nikisema tu nitakufa .
Na Alice nae alisema hivyohivy, nilibakia tu kuwa mpole na kuacha afanye anavyojua yeye. vituko vilianza pale nyumbani, Alice alianza vituko. kuna Siku alikuwa anatenga chakula akiwa uchi wa mnyama na mimi tu ndiye nilikuwa namuona wengine walikuwa hawaoni hali ile.
Siku moja ilikuwa asubuhi sana Dada yangu alikuja kuniamsha na kunitaka niende ubungo kwa ajili ya kukata tiketi ya bus ambapo shemeji alikuwa akitaka kusafiri kuelekea Mwanza
Niliamka na kujianda kwa ajili ya kwenda ubungo , nilienda kupanda gari na kuelekea ubungo huku nyumbani Alice alibakia pekee yake na kazi zilikuwa nyingi kidogo maana maji yalikata hivyo ikabidi achote kwa jirani yetu wakati anachota yale maji huku nyumbani kulikuwa kazi ya kuosha vyombo na kudeki ndani mimi nilienda nikakata tiketi nivyorudi niliona maajabu sana kusema ukweli.
Nilingia ndani nikamkuta Alice anadeki nikamsalimia ,nilivyotoka nje nikamkuta anaosha vyombo wakati bado nazubaa na kushangaa nikamuona amebeba ndoo ya maji hapo mimi nilichanganyikiwa maana alikuwa amejigawa Mara tatu na wote walikuwa wanafanya kazi!.....
je nini kiliendelea ?SHARE TUZIDI KUSONGA MBELE.
Previous Post
Next Post

0 Comments: