Friday, March 8, 2019

Vickekesho na Vituko vya Uzamiaji wa Kwenye Misiba

Vickekesho na Vituko vya Uzamiaji wa Kwenye Misiba
Tokeo la picha la msibani
Hapa duniani vituko haviachi kwisha, jamaa mmoja alitoa kichekesho cha mwaka katika moja ya uzamiaji wake wa kwenye misiba kutoka Arusha, siku moja katika pitapita yake aliingia mtaa mmoja na katika kutembea kidogo akakutana na nyumba yenye msiba.
Jamaa kama kawaida yake akazamia na kwa bahati nzuri akakuta ndo waombolezaji waliokuwa wamekesha hapo walikuwa wanapata uji wa moto ili kufukuza baridi. Jamaa naye yumo akapata kikombe chake na kwa bahati mbaya akapaliwa na uji wa moto kiasi cha kutokwa na machozi. Wale wenzake msibani wakaanza kumpa pole.
Ili kupotezea kwamba hajaunguzwa na uji akaanza kusema (huku akionekana analia kwa sababu ya yale machozi)
“MAREHEMU ALIKUWA MTU MZURI SANA” “YAANI ALIKUWA ANAPENDA WATU” “TAIFA LIMEPOTEZA TUNU MUHIMU SANA” “MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI”.
Kumbe aliyekuwa anazikwa ni katoto ka siku moja tu! Wazamiaji bwana!!
Continue reading

Thursday, March 7, 2019

Cheka na Bwana Harusi Kikojozi

Cheka na Bwana Harusi Kikojozi

Tokeo la picha la Bwana Harusi anakojoa
Jamaa alikuwa ana tabia ya kukojoa kitandani baadhi ya siku.
Akafikia kuoa. Katika ya siku za mwanzo baada ya harusi, siku moja kama kawaida yake alijikojolea.
Akapiga kelele “Mungu wangu eee”.
Mke wake akashtuka, akamuuliza: Vipi mume wangu?
Mume: Hivi mke wangu ungeota unataka kuliwa na mamba, chuwi na simba kwa wakati mmoja ungefanyaje?

Mke: Ningezimia kabisa.Mume: Basi mwenzio sijazimia nimejikojolea.

Continue reading

Kuna mambo mawili yatakuhusu maishani

Kuna mambo mawili yatakuhusu maishani
Tokeo la picha la TO FINGURE
Kuna mambo mawili ukizaliwa na kuishi yatakuhusu
  1. Ni ama wewe utazaliwa mwanaume
  2. Au wewe utazaliwa  mwanamke
Kama wewe utazaliwa mwanamke uko salama,
Lakini kama wewe utazaliwa mwanaume kuna mambo mawili yatakuhusu
  1. Aidha wewe utaajiriwa uraiani
  2. Au utaajiriwa jeshini
Kama wewe utaajiriwa uraiani uko salama,
Lakini kama wewe utaajiriwa jeshi kuna mambo mawili yatakuhusu
  1. Aidha wewe utafanya kazi za ofisini
  2. Au utafanya kazi za mstari wa mbele vitani
Kama wewe utafanya kazi ofosini uko salama,
Lakini kama wewe utafanya kazi mstari wa mbele vitani kuna mambo mawili yatakuhusu
  1. Aidha wewe utaua
  2. Au Utauawa
Kama utaua mtu uko salama,
Lakini kama utauawa kuna mambo mawili yatakuhusu
  1. Aidha mwili wako utazikwa
  2. Au mwili wako utatumika kama mbolea.
Kama mwili wako utazikwa uko salama,
Lakini kama mwili wako utatumika kama mbolea kuna mambo mawili yatakuhusu.
  1. Aidha wewe ni itatumika kwa kupanda maua
  2. Au utatumika kupanda miti.
Kama ilitumika kwa kupanda maua uko salama,
Lakini kama itatumika kwa kupanda miti kuna mambo mawili yatakuhusu.
  1. Ni ama zitatumika kutengeneza karatasi za kutumia chooni
  2. Au itatumika kutengenezea samani za ofisini na majumbani.
Kama zitatumika kutengeneza samani za ofisini na majumbani ni salama,
Lakini kama zitatumika kutengeneza karatasi za chooni kuna mambo mawili zitahusisha
  1. Aidha zitatumiwa na mwanaume
  2. Au zitatumiwa na mwanamke
Kama zitatumiwa na mwanaume ni salama,
Lakini kama zitatumiwa na mwanamke kuna mambo mawili yatakuhusu
  1. Aidha zitatumika kusafisha upande wa nyuma
  2. Au zitatumika kusafisha upande wa mbele
Kama zitatumika kwa nyuma uko salama
Lakini kama zitatumika kwa mbele malizia mwenyewe mambo mawili yatakayotekea…
Continue reading

Mchaga Kwenye Kisima

Tokeo la picha la kisima cha maji
Mtoto: Baba ebu daka hiyo kamba uing’ang’anie ili tukuvute mpaka utoke uko

Baba wa kichaga: Kwani hiyo kamba umenunua shilingi ngapi na kwa nani?

Mtoto: Nimenunua Shilingi elfu moja kwenye lile duka la mpare

Baba wa Kichaga: Alipatwa na mshangao haraka akajibu, Eyowii!! Amekuuzia ghali sana kijana, ebu rudisha na ukanunue kamba kwa Mosha anauza mia tano.
Continue reading

Vichekesho vya Mmasai na Basi la Abiria

Tokeo la picha la wamasai
Kulikuwa na basi moja la abiria likitokea Dar es salaam kwenda morogoro, baada ya kupita Chalinze kama kilomita 50 hivi, utingo wa basi alimuona abiria wa kimasai akisimamisha basi. Hapo utingo kwa haraka alimuashiria dereva asimamishe basi ili waongeze abiria.

Cha kuchekesha ni hii, mmasai baada ya kuingia ndani ya basi kwa ujasiri kabisa aliomba kama kuna abiria mwenye kiberiti ili awashe msokoto wake wa sigara.

Basi zima likaangukia kucheka na kunjika mbavu akiwemo dereva na konda.

Continue reading

Baba mzee mkongwe kuliko wote duniani

Baba mzee mkongwe kuliko wote duniani
Baba mzee mkongwe kuliko wote duniani

Binadamu wa kihindi ambaye ndie baba mzee mkongwe kuliko wote duniani kawa baba kwa mara ya pili akiwa na umri wa miaka 96.

Raghav Ramjit ilitunukiwa kuwa baba mzee mkongwe kupita wote dunbiani miaka miwili iliyopita wakati yeye alikuwa amemzaa mwana wake wa kwanza Karamjit akiwa na umri wa miaka 94.

• Pamoja na uzee na ukongwe wake Ramjit Raghav ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa mara tatu kwa usiku mmoja
• Mwanawe wa kwanza, Karamjit, alizaliwa miaka miwili iliyopita katika mji wa Haryana, kaskazini mwa India
Continue reading

Misemo ya Wabunge Bungeni Tanzania

Misemo ya Wabunge Bungeni Tanzania
Tokeo la picha la bunge la tanzania
je wajua hii misemo ya wabunge bungeni?
Wabunge wa bunge la Tanzania kwa nyakati tofauti ndani na nje ya bunge wamekuwa wakitoa misemo mbalimbali na ya ajabu yenye kujenga, kubomoa na kuchekesha kila mtu aliyesikia, ona kwa macho au kupitia TV au kusoma magazetini
Rais ni Mdhaifu
-John Mnyika
Tumefika hapa tulipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais
-John Mnyika
Problems cannot be solved by the same level which create them
-Mch. Peter Msigwa
Mchungaji wa Mbuzi na Kuku
-Mangunga
F. U. C. K , You
-Serukamba
Rais ndiye chanzo cha vurugu za kidini
-Godbless Lema
Dhambi mbaya kuliko zote duniani. Ni woga
-Godbless Lema
Waziri mkuu aliidanganya serikali
-Godbless Lema
Wapinzani wanangoa watu kucha na meno
-Manyanya na Mwingulu
Siongei na mbwa naongea na mwenyembwa
-Nkamia.
Wapinzani ni wahuni
-Samwel Sitta
Mhuni ni wewe mwenye kadi mbili ya CCM na CCJ
– Upinzani – CHADEMA
Wanaume wanapoongea watoto wakiume wakae chini
Mwigulu Nchemba
Continue reading